HUU NI UKAUZU KWA KWELI....KAMA NI
WEWE UNGEFANYAJE??
Baada ya miaka minne ya kuajiriwa
bila hata kuongezwa mshahara au hata marupurupu, Bwana Saadaty Hassani aliamua
kwenda kwa bosi wake kulalamika.
Jibu alilolipata kwa bosi wake ni
kwamba hakupewa nyongeza wala marupurupu kwa sababu HAKUSTAHILI.
Akauliza kwa nini?
Akaambiwa katika miaka minne
uliyofanya hapa, hujafikisha mwaka hata mmoja.
Akasimama na kuanza kufoka,
akaambiwa kaa chini, na majibizano yakawa hivi;
Bosi; Mwaka una siku ngapi?
Saadaty: 365 au 366.
Bosi: Huwa unakuja kazini wikiendi?
Saadaty: Hapana
Bosi: Hebu piga hesabu mwaka una
jumamosi na jumapili ngapi kisha zitoe katika 366
Saadaty: Jumamosi 52 na Jumapili 52
jumla unapata siku 104. Ukitoa katika siku 366 unabaki na siku 262.
Bosi: Siku ina masaa 24, wewe
unafanya kazi masaa mangapi?
Saadaty: Masaa nane kwa siku
Bosi: Sasa nipigie hesabu masaa nane
katika masaa 24. Nane kwa 24 inaingia mara ngapi?
Saadaty: Inaingia mara tatu mkuu
Bosi: Sasa ukizigawa zile siku 262
kwa masaa uliyofanya kazi yaani uigawe kwa tatu kulingana na masaa uliyofanya
kazi unapata siku ngapi zilizokamilika?
Saadaty: 87
Bosi; Kwa mujibu wa saa ulizofanya
kazi kwangu, ni sawa na siku 87, tuendelee na mahesabu?
Saadaty: Tuendelee
Bosi: Unakumbuka uliumwa wiki mbili
nikakupa likizo? Na ulishachukua likizo yako ya kawaida siku 28 na ukaenda
msibani wiki moja hebu piga hesabu vizuri.
Saadaty: 14 + 28 + 7 = 49
Bosi; Toa katika siku 87
Saadaty: 42
Bosi; Toa sikukuu za Idd, Maulid,
Uhuru, Mapinduzi, Pasaka, Krismas, Nyerere Day, Mwaka mpya, Mei Mosi, Sabasaba,
Nanenane na ile wiki iliyonyesha mvua kuuubwa nikawaruhusu mpumzike.
Saadaty: Bosi naomba nikaendelee na
kazi
Bosi: Malalamiko vipi?
Kuwa bosi wako mwenyewe....
Fanya kazi kwa muda na masaa
unayotaka wewe...
Amka muda unaotaka wewe baada ya
usingizi kuisha sio muda unaolazimika kwa sababu uzijuavyo....
Tumia muda wako vizuri.....masaa 8
fanya kazi,8 mengine ni ya kupumzika nikimaanisha kulala na yaliyobakia fanya
kitu ambacho kitakuzalishia au kukuletea kipato endelevu......
mtegemea cha bosi pekee hufa
masikini wakati wengine wanatambua fursa mbalimbali wanzaokutana nazo na
kuzifanyia kazi wanafanikiwa sana kufikia mahali wanapohitaji kuwa na majina
yao yanabadirika ,mfano wao ni akina REGINALD MENGI,SAALIM BAKHRESA,MOHAMED
DEWJI ,MILLARD AYO,ERICK SHIGONGO,PAUL BISWALO na wengine wengi hapa tanzania.
*........KAMA WEWE UPO HIVYO
BADILIKA.............
HUU NI WAKATI WA KUWAFUNDISHA WATU
UKWELI ILI WAPATE KUFANIKIWA PASIPO KUTEGEMEA AJIRA PEKEE ETI ZITAWAFANIKISHA
WAKATI UKWELI NI KWAMBA AJIRA NI MTEGO WA KUFANIKIWA KATIKA MAISHA YA WAJIRIWA
NA KUSHINDWA KUISHI NDOTO ZAO MAANA ZINAWABWETESHA AKILI NA KUZIFANYA KUWA
MGANO NA KUISHI MAISHA YA KIMASIKINI KABISA.
e.t.c.........................................*
Umaskini sio hali ya kukosa mali na
kuwa na hali duni, umasikini ni mtazamo usioweza kuzalisha, usiowaza
kufanikiwa, usiotaka kujituma.
Ebu pokea hili wazo la utajiri upate
kufanikiwa, na wewe uliyefanikiwa acha kuwaza kimaskini.
Yupo maskini mwenye mawazo ya
utajiri, na yupo tajiri mwenye mawazo ya kimaskini tumia utajiri wako kwa ajiri
ya kazi ya BWANA.
ZIFUATAZO NI SIRI SITA AMBAZO
MWAJIRIWA HAZIFAHAMU ZINAZOWAFANYA WASIISHI NDOTO ZAO NA BADALA YAKE WANAISHI
NDOTO ZA BOSI WAKE.
1)kuanza safari ya maisha bila kuwa
na ramani ya uendako.
2)kuwaza pesa kuliko kuwaza wazo la
kukuingizia pesa,hapa mtu yuko tayari kuajiriwa alipwe kiasi kidogo tu cha pesa
mwisho wa mwezi kuliko kufanya shughuli zake mwenyewe kisa eti mshahara upo
kila mwezi na akifanya mambo yake binafsi hayamhakikishii kupata pesa katika
maisha yake kwa wakati.
3)kutokujua kuwa kipato chako
kinategemeana na thamani au mchango wako sokoni.wakati ukiangalia pesa
unayolipwa haiendani kabisa na elimu yako na ujuzi wako.
4)ukosefu wa mpango endelevu wa
kurithisha kizazi baada ya kizazi,hapa unamkuta mtu anaringa na cheo chake
utafikiri atamuachia mwanae wakati hatima ya maisha yake yako kwa bosi na
akifukuzwa hana kitu hata watoto wake pia watajitafutia kila kitu mpaka kuja
kufikia cheo kama cha mzazi wake.
5)kufikiri kunakoongozwa na hofu
badala ya ndoto,anahofia kufukuzwa kazi tu muda wote anaacha kuwaza ndoto zake
maana pia ukitazama pesa anayopata ni ndogo sana kulinganisha na muda aliowekeza
kwa bosi na sio kwa mambo yake binafsi.
6)kukosa uelewa wa ujengaji utajiri
wa ukweli ,hapa utakuta mtu anaamua kujilimbikizia mali eti kisa rafiki yake
kafanikiwa yeye hakuna ,utamkuta anakula rushwaili aje kuwa tajiri mwisho wa
siku anaishia jela.
Haya ndio wajiriwa wengi hawajui
,wanaishia kuringi cheo chake ,nikwambie tu cheo ni dhamana na pia nikama nguo
ya kuazima mwenye nayo akija anahitaji nguo yake haijalishi umekutananaye
maeneo gani,utaumbuka akianza kukuvua nguo yake na ukweli watu wataufahamu
ukiwa uchi kama ulivyozaliwa baada ya nguo kuchukuliwa na mwenye nao.
Tafuta kitu cha ziada ufanye kwa
muda wako wa ziada,na kama hujui nini cha kufanya wasiliana na mimi
nitakusaidia ufanye nini ili uishi maisha ya ndoto zako kwa kupitia namba hii
+255768603979.
" Change your MIND, before you
change your LIFE ".
*YOU ARE WHO YOU ARE BECAUSE OF YOUR
MIND*..!
Jipatie nakala yako ya #BE EMPLOYED
WITH PLAN "B",unaweza kuweka oda yako mapema kupitia namba hii
+255768603979,ili uepukane na mawazo mgando yakulalamika bila kufikia ndoto
zako wakati wengine wanaopenda kusoma vitabu wanapata mawazo na mbinu mpya za
kufanikiwa na maisha yanakwenda vizuri.
wako katika kuijenga imani yako juu
ya kufanikiwa katika jambo unalohitaji katika maisha yako,
-Paul Biswalo.
Mhamasishaji,Muelimishaji,Mkufunzi,Mwalimu.
(Mwenye Vipaji Vingi/Asiyekuwa na
Kikomo).
#Badilika#
#Shtuka#
#Amka#
#HapaKaziTu.