Health And Wellness Is Your Priority & Personal Development Mentorship Programs.

“Your health is your responsibility, love your health as you love your stuff”. -@Paul Biswalo.

We are looking forward to connect with you.

Our phone number is +255 768 603 979,for only calls/text &
+255 ,for WhatsApp only.
Email-address : biswalopaul@gmail.com.

It's me your lovely friend,
Yours in faithfulness,

-@Paul Biswalo, C.E.O & FOUNDER.
Mentor || Motivational Speaker || Trainer || Event Host || Entrepreneur || Healthy & Life coach || Presenter & Inspirational Public Speaker.
*let's meet all at the Top because is no longer crowded*

FAHAMU UGONJWA WA KUVIMBA KWA TEZI DUME (BENIGN PROSTATE HYPERPLASIA BPH) FEATURE NA MATIBABU YAKE.USITAMANI KUFA KWANI KILA TATIZO LINA SULUHISHO LAKE





KUVIMBA KWA TEZI DUME (BENIGN PROSTATE HYPERPLASIA BPH) FEATURE
Ni matumaini yangu unaendelea vyema mpendwa msomaji wa blog yetu hii ya Health and wellness is your priority & personal development mentorship programs.

Naam ni jambo la kumshukuru Mwenyezi MUNGU kuiona siku mpya kila siku haijalishi unaumwa ama una magumu unapitia USITAMANI KUFA KWANI KILA TATIZO LINA SULUHISHO LAKE hivyo mshukuru Mwenyezi MUNGU kwa kila kitu katika maisha yako.

Ama baada ya salam Leo ni vyema tukapata darasa kuhusiana na kichwa cha habari hapo juu

 
TEZI DUME (PROSTATE GLAND).
Tezi dume ni sehemu mojawapo ya mfumo wa uzazi wa kiume. Inaundwa na sehemu mbili, lobes, ambazo zimeunganishwa na kufunikwa kwa nje kwa utando wa tishu. Tezi hii ipo mbele kidogo ya puru (rectum) na na chini kidogo ya kibofu cha mkojo. Tezi dume inauzunguka mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na uume (urethra).

Mojawapo ya kazi za tezi dume ni kutoa majimaji yanayochanganyika na mbegu za kiume (sperms) wakati wa kilele cha tendo la ngono. Mchanganyiko huu wa mbegu pamoja na majimaji hayo hufanya shahawa (semen). Aidha majimaji hayo husaidia kuzipa mbegu za kiume nguvu ya kusafiri kwenye uke mpaka kufikia kwenye mirija ya fallopian tayari kwa utungisho na yai la kike. Vilevile husaidia kupunguza hali ya kitindikali iliyopo katika uke, ambayo kama isiporekebishwa, huweza kuua mbegu nyingi za kiume na kufanya utungisho kuwa wa tabu.

KUVIMBA TEZI DUME (BPH)
Kwa kadiri mwanaume anavyozeeka, ni jambo la kawaida pia kwa tezi dume kuongezeka ukubwa na kuvimba. Hali hii kitabibu huitwa Benign Prostate Hyperplasia au wengine hupenda kutumia maneno Benign Prostate Hypertrophy kwa kifupi BPH. Kwenye makala hii tutautumia sana ufupisho huu wa BPH ili kurahisisha mambo.

 
Ukuaji wa tezi dume hupitia hatua kuu mbili. Hatua ya kwanza hutokea kipindi cha balehe wakati tezi dume linapoongezeka ukubwa na kuwa mara mbili ya lilivyokuwa hapo awali. Baada ya hapo ukuaji husimama kwa muda mpaka kijana anapofikisha miaka 25 hadi 30 ndipo hatua ya pili ya ukuaji huanza tena. Ukuaji huendelea kwa viwango na kasi tofauti kati ya mtu na mtu na hatimaye kusababisha BPH katika umri wa utu uzima.

 

Wakati tezi dume linapokua na kutanuka, utando wa tishu unaozulizunguka hutanuka pia. Hata hivyo ingawa tezi dume huendelea kukua, hufikia wakati utando wake huacha kutanuka na kufanya tezi dume kubana mrija wa kutolea mkojo kutoka kwenye kibofu. Hali hii husababisha kibofu cha mkojo kuwa na ngozi ngumu. Hali hii hufanya kibofu cha mkojo kuhisi kutaka kutoa mkojo nje hata kama kiasi cha mkojo ndani yake ni kidogo sana. Hufikia wakati, kibofu huwa dhaifu na kupoteza uwezo wake wa kuhisi kutoa mkojo na hivyo kufanya mtu anapokojoa kushindwa kutoa mkojo wote na badala yake hubakiza kiasi fulani cha mkojo kwenye kibofu.
 

CHANZO AMA VYANZO VYA KUPATA BPH:
Chanzo halisi cha BPH au vihatarishi vyake (risk factors) havijulikani kwa uhakika. Kwa muda mrefu imekuwa ikichukuliwa kuwa BPH hutokea kwa wanaume watu wazima na wazee tu. Aidha imewahi kuonekana huko nyuma kuwa PBH haitokei kwa wanaume ambao wamewahi kufanyiwa operesheni ya kuondoa korodani au wale ambao walizaliwa bila korodani. Hali imepelekea baadhi ya watafiti kuamini kuwa BPH ina uhusiano mkubwa na umri wa mtu pamoja na uwepo wa korodani.
Kuna dhana (theories) kadhaa zinazojaribu kuelezea chanzo cha BPH. Dhana hizo ni pamoja na

UHUSIANO KATI YA BPH NA HOMONI YA ESTROGEN:
Wanaume huzalisha testosterone, homoni ya muhimu sana katika mwili wa mwanaume. Hali kadhalika huzalisha pia estrogen ambayo ni homoni ya kike kwa kiwango kidogo sana. Kadiri jinsi mtu anavyozeeka, ndivyo uzalishaji wa testosterone unavyokuwa mdogo na kufanya kiwango chake katika damu kupungua kulinganisha na kiwango cha estrogen ambacho huongezeka kwa kiasi fulani. Pamoja na kazi nyingine, estrogen pia huchochea ukuaji wa chembe hai za mwili. Tafiti zilizofanywa kwa wanyama zimeonesha kuwa BPH hutokea kwa sababu kiwango kikubwa cha estrogen katika damu huchochea ukuaji wa seli za tezi dume na hivyo kufanya tezi dume kuvimba.

UHUSIANO KATI YA BPH NA DIHYDROTESTOSTERONE (DHT):
DHT ni kiasili kinachozalishwa kutokana na testosterone kwenye tezi dume, ambacho husaidia kuthibiti ukuaji wa tezi dume. Ingawa wanyama wengi hupoteza uwezo wa kuzalisha DHT wanapofikia umri wa uzee, baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa, kwa binadamu, hata kama kiwango cha testosterone kitapungua sana katika

damu, wanaume watu wazima bado wana uwezo wa kuzalisha kiasili hiki cha DHT katika tezi dume zao. Uzalishaji na uklimbikaji huu wa DHT huchochea kwa kiasi kikubwa ukuaji wa seli za tezi dume na kusababisha BPH. Wanasayansi wamegundua kuwa wanaume watu wazima wenye
kiwango kidogo cha DHT hawapati BPH.

UHUSIANO KATI YA BPH NA MAELEKEZO YA SELI:
Dhana nyingine inasema kwamba baadhi ya seli kutoka katika sehemu fulani ya matezi yanayohusika na ukuaji mwilini hupewa maelekezo wakati mtu anapokuwa bado mdogo. Seli hizi hutunza maelekezo hayo na baada ya miaka kadhaa maelekezo haya huanzwa kutekelezwa na seli za matezi mengine. Mojawapo ya melekezo hayo ni kuchochea ukuaji wa tezi dume na kusababisha BPH.



DALILI ZA BPH:
Dalili za BPH hutokea kwa sababu ya kubanwa kwa njia ya kutoa mkojo nje ya mwili (urethra) au kibofu kushindwa kuthibiti mkojo. Aidha dalili hizi hutofautiana kati ya mtu na mtu, ingawa karibu wagonjwa wote
  1. Hukojoa mkojo unaokatika katika
  2. Hukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu
  3. Husita kabla ya kuanza kukojoa
  4. Hali ya kujihisi kubanwa na mkojo kila mara
  5. Kushindwa kuthibiti mkojo kiasi cha mkojo kutirika wenyewe
  6. Hali ya kuhisi mkojo haujaisha kwenye kibofu
  7. hukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku
  8. Kushindwa kukojoa kabisa (urine retention)
  9. Au dalili zinazotokana na madhara ya BPH
MADHARA YA BPH
BPH kama ilivyo saratani ya tezi dume, inaweza kumletea mgonjwa madhara (complications) kadhaa. Madhara hayo ni pamoja na
  1. Mkojo kushindwa kutoka (retention of urine)
  2. Mgandamizo kwenye kibofu cha mkojo
  3. Vijiwe kwenye kibofu cha mkojo
  4. Uambukizi katika njia ya mkojo (UTI)
  5. Madhara katika figo au kibofu
  6. Shinikizo la damu
  7. Kushindwa kutoa shahawa kwenye uume (retrograde ejaculation)
  8. Maambukizi mbalimbali
  9. Nimonia (Pneumonia)
  10. Damu kuganda
  11. Uhanithi
VIPIMO NA UCHUNGUZI WA BPH.
Baada ya mgonjwa kujihisi dalili zilizotajwa hapo juu, daktari atamfanyia uchunguzi wa mwili kabla ya kumfanyia vipimo zaidi. Vipimo vyaweza kutofautiana kati ya mgonjwa namgonjwa, lakini baadhi ya vipimo ni pamoja na
Kuchunguza Tezi Dume kupitia njia ya haja kubwa au

DIGITAL RECTAL EXAMINATION (DRE): Hiki ni kipimo cha kwanza kabisa ambacho mgonja hufanyiwa na daktari wake. Ni kipimo kinachoweza kumpa daktari picha ya tatizo na kufahamu kuhusu ukubwa na hali ya tezi dume. Daktari akiwa amevaa glovu huingiza kidole chake cha shahada katika njia ya haja kubwa au puru (rectum) ya mgonjwa kasha kuzungusha zungusha ili kufahamu kama tezi limevimba ama la na pia hali yake
kama ni gumu kuliko kawaida ama lina utando na nyama laini.


KIPIMO CHA DAMU CHA PROSTATE-SPECIFIC ANTIGEN (PSA): PSA husaidia kutofautisha kati ya saratani ya tezi dume na BPH. PSA ni aina ya protein inayozalishwa na seli za tezi dume na kiwango chake huongezeka iwapo kuna saratani ya tezi dume.

ULTRASOUND YA PURU (RECTAL ULTRASOUND): Kipimo hiki hufanyika iwapo daktari atahisi kuwepo kwa saratani ya tezi dume badala ya BPH. Utrasound ya puru pamoja na kuonesha taswira ya tezi dume ilivyo, pia humuwezesha daktari kuchukua kinyama (biopsy) kwenye tezi dume kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kutofautisha kati ya saratani na BPH.

KIWANGO CHA UTOKAJI WA MKOJO(URINE FLOW STUDY): Ni kipimo kinachotumika kufahamu kasi ya utokaji wa mkojo. Mkojo unaotoka kwa kasi na kiwango kidogo huashiria kuwepo kwa BPH.

KIPIMO CHA KUCHUNGUZA KIBOFU CHA MKOJO(CYSTOSCOPY): Kipimo hiki husaidia kuweza kufahamu ukubwa wa tezi, sehemu tezi lilipobana njia ya mkojo na kiwango cha kubana huko. Aidha huwezesha pia kutambua hali ya kibofu cha mkojo ikoje.

MATIBABU YA BPH
Matibabu ya BPH yameganyika katika sehemu mbili, yale yanayofanywa kwa kutumia dawa na yale yanayofanywa kwa kutumia upasuaji mdogo. Aidha matibabu hufanywa kwa watu wenye BPH kubwa zaidi na dalili zinazowaletea usumbufu na kuathiri maisha yao, wakati wale wenye dalili ndogo ndogo hawalazimiki sana kuhitaji matibabu.

MATIBABU KWA NJIA YA DAWA
Dawa hizi hutumika kwa lengo la kulifanya tezi dume kusinyaa na kupungua ukubwa wake. Dawa hizo ni pamoja na
Finasteride na dutasteride ambazo huzuia uzalishajiwa homoni ya DHT. Matumizi ya dawa hizi husaidia kuzuia kukua na kuvimba kwa tezi dume au kulifanya tezi dume kusinyaa kabisa kwa baadhi ya wanaume.
Terazosin, doxazosin, tamsulosin na alfuzosin husaidia kulainisha misuli ya tezi dume na hivyo kupunguza mbano wa mrija wa urethra, hali inayosaidia mkojo kutoka vizuri.

MATIBABU KWA NJIA YA UPASUAJI
Upasuaji mdogo (minimal Invasive procedures)
Upasuaji mdogo husaidia kuondoa dalili za BPH na hufanyika pale ambapo matibabu kwa njia ya dawa yameshindwa kuonesha mafanikio yeyote. Njia hizo niTiba ya kutumia mawimbi ya joto (Transurethral microwave procedures, TUMT): Tiba hii hutumia kifaa kinachotoa mawimbi ya joto (microwave) yanayochoma na kuharibu tishu zilizovimba za tezi dume.

Matibabu huchukua chini ya saa moja na yanaweza kufanyika bila mgonjwa kuhitaji kulazwa.Tiba ya kutumia sindano maalum (Transurethral needle ablation, TUNA): Njia hii hutumia visindano vidogo ambavyo huunganiswa kwenye chombo chenye kutoa nishati ya joto kuunguza tishu zilizovimba za tezi dume.

Tiba ya kutumia joto la maji (Water-induced thermotherapy): Tiba hii hutumia maji ya moto yaliyochemshwa kwa kifaa maalum kuunguza na kupunguza tishu zilizovimba za tezi dume.
Madaktari wengi hushauri kuondolewa kabisa kwa tezi dume iwapo itathibitika kuwa mgonjwa ana BPH. Zipo njia nyingi za upasuaji wa BPH, nazo ni pamoja na upasuaji kwa kupitia kwenye mrija wa mkojo (Transurethral surgery, TURP), upasuaji mkubwa wa wazi (Open surgery), upasuaji wa kutumia nishati kuondoa tishu za tezi dume Laser surgery), na upasuaji wa kutumia joto la fibreoptic probe kuchoma tishu za tezi dume (Interstitial laser coagulation).

Vitu vya kufanya baada ya Upasuaji wa Tezi dume.
  • Mara baada ya upasuaji wa tezi dume inashauriwa
  • Kunywa maji kwa wingi ili kusafisha kibofu cha mkojo
  • Epuka kujikakamua sana unapojihisi kwenda haja kubwaKula lishe bora ili kuepuka kupata choo kigumu. Iwapo mgonjwa atapatwa na choo kigumu ni vyema amuone daktari ili amshauri jinsi ya kuondoa tatizo.
  • Epuka na acha kunyanyua vitu vizito.
  • Hairuhusiwi kuendesha gari wala kuendesha mtambo wowote ule mpaka utakapopona kabisa.Matatizo yanayoweza kutokea baada ya upasuaji
SHIDA WAKATI WA KUKOJOA: Kawaida huchukua muda wa siku kadhaa mtu kuweza kurejea katika hali yake ya kawaida ya kukojoa.

SHIDA YA KUTHIBITI MKOJO USITOKE OVYO (INCONTINENCE): Ni kawaida kwa mgonjwa kushindwa kuthibiti kutoka kwa mkojo katika siku za mwanzo baada ya operesheni. Hata hivyo hali hii hujirekebisha baada ya siku kadhaa kupita.Kutokwa na damu: Katika siku za wali mara baada ya TURP, kidonda kwenye tezi dume kinaweza kuvuja damu ambayo itaonekana katika mkojo.

Hata hivyo hali hii hukoma baada ya wiki kadhaa. Hata hivyo iwapo utokaji damu ni mzito sana, inashauriwa kumuona daktari haraka.Uwezo wa kufanya ngono baada ya upasuaji
Wagonjwa wengi waliofanyiwa upasuaji wa BPH uhofia sana kuhusu uwezo wao wa kufurahia tendo la ngono mara baada ya upasuaji. Kwa kawaida, huchukua muda fulani kwa agonjwa kuweza kurejea hali ya kawaida ya kufurahia tendo hili.

MDISO AU KUDINDISHA (ERECTIONS): Madaktari wengi husema kuwa iwapo mgonjwa aliweza kupata mdiso au kudinda muda mfupi baada ya upasuaji, uwezo wake wa kuendelea kupata mdiso ni mkubwa zaidi. Hata hivyo iwapo mgonjwa hakuwa na uwezo wa kudisa tangu awali, upasuaji wa tezi dume hauna uwezo wa kumrejeshea uwezo wake wa kudisa.Kutoa mbegu (Ejaculation):

Ingawa wanaume waliofanyiwa upasuaji wa tezi dume bado wanaweza kupata mdiso, mara nyingi upasuaji huu huwafanya wawe wagumba yaani wasioweza kupata watoto. Hali hii kwa kitaalamu huitwa retrograde ejaculation au kilele (mshindo) kikavu (dry climax). Kwa kawaida, wakati wa tendo la ngono, mbegu za kiume kutoka kwenye korodani huingia kwenye urethra
karibu na kijitundu cha kibofu cha mkojo.

Wakati wa tendo la ngono, misuli maalum hufunga kijitundu hicho ili kuzuia mbegu zisiingie kwenye kibofu badala yake zielekee kwenye urethra ya katika uume. Hata hivyo, upasuajiwa BPH huondoa misuli hiyo na kufanya mbegu kuingia
kwenye kibofu cha mkojo badala ya kuendelea kwenye urethra ya uume. Shahawa hizo hatimaye hutolewa nje ya kibofu pamoja na mkojo.Kufika kilele (Orgasm): Huwa hakuna tofauti kubwa ya kufika kilele (orgasm) kabla na baada ya kufanyiwa upasuaji.

na SARATANI YA TEZI DUME: Hakuna Uhusiano wa moja kwa moja Ingawa baadhi ya dalili za BPH zinafanana na zile za saratani ya tezi dume, kuwa na BPH hakuongezi uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume. Hata hivyo, mwenye BPH anaweza pia na saratani ya tezi dume bila saratani hiyo kugundulika, ama wakati huo huo au siku za baadaye. Hivyo inashauriwa kuwa, ni vema wanaume wote kuanzia miaka 40 na keundelea kufanya uchunguzi wa tezi dume zao walau mara moja kwa mwezi.
 


MATIBABU YA TEZI DUME CHINI YA UONGOZI WA HEALTH AND WELLNESS IS YOUR PRIORITY CONSULTANTS.

Mpendwa msomaji wa blog yetu tunakukaribisha kwa ajili ya ushauri nasaha pamoja na matibabu ya kutumia Virutubisho asili kama vile :bee propolis, abeta-carotene, l-arginine, garlic thyme, omega-3, stabilized aloe, malti-minerals, vitolize for men na licium plus.

Matibabu ya tezi dume katika ofisi yetu ni matibabu ya kutumia Virutubisho asili ambazo utapatiwa kutokana na hali yako ya kiafya jinsi ilivyo .
Zifuatazo ni baadhi ya virutubisho zinazotumika kuondoa tatizo la tezi dume kwenye afya yako.
 

A].BEE PROPOLIS.
Kirutubisho hiki ni cha kiasili kimetengenezwa kwa kutumia viambata vifuatavyo
Rhamnocitrin, pterostilbene, xanthorrhoeol, pectolinarigenin, vanillin, 3-acetyl pinoban, n.k.

KAZI NA FAIDA YA HIKI KIRUTUBISHO.
  • Kuboresha mzunguko wa damu ndani ya tezi dume
  • Kuzuia kuzaliana kwa wadudu wabaya ndani ya tezi dume
  • Kuondoa dalili za matatizo ya tezi dume
  • Vitolize for men Inafaa kwa mwanamme mwenye tatizo lolote la tezi dume na inawafaa Wanaume wenye umri unaozidi miaka 40 kwaajili ya kujikinga na tezi dume.
BEE PROPOLIS INASAIDIAJE KWA MWENYE TEZI DUME?
Kirutubisho hiki kinazuia na kuondoa dalili za matatizo ya tezi dume kama, kukojoa kila mara, mkojo kutoka kwa shida au maumivu wakati wa kukojoa. bee propolis inaboresha mzunguko wa damu na kuzuia ukuaji wa vijidudu wadogo wanaoweza kusababisha maambukizi katika tezi dume.


B].ABETA-CAROTENE & LICORICE CAPSULES.
Kirutubisho hiki ni cha kiasili kimetengenezwa kwa kutumia viambata ambavyo ni B_carotene na licorice.

KAZI NA FAIDA YA HIKI KIRUTUBISHO.

  • Huurutubisha mwili na kuongeza vitamini A
  • Hufanya kazi kama antioxidant yenye nguvu na kuondoa radikali huru
  • Huzuia na kutibu kansa na hasa kansa ya tezi dume
  • Huzuia na kutibu atherosclerosis kwa kupunguza lipids kwenye damu 

KIRUTUBISHO HIKI KINAFAA KUTUMIWA NA
Watoto na watu wazima wenye upungufu wa vitamini ‘A’Wanaume wenye matatizo ya tezi dume kama prostatitis, tezi iliyovimba (BPH), na kansa ya tezi dumeWatu wenye uwingi wa lipids ndani ya damu.

UFANYAJI KAZI WA B-CAROTENE KAMA VITAMINI ‘A’.
B-carotene ni rangi ya asili (nyekundu-rangi ya chungwa) ndani ya karoti inayozifanya kuwa na rangi ya chungwa na ndiyo namna carotene inavyokuwa katika mimea. Molekuli moja ya B-carotene huweza kuvunjwa na vimeng'enya vilivyoko ndani ya utumbo na kupata molekuli mbili za vitamini A, ambayo huchochea kujigawa kwa seli, husaidia mwili kukua, na huongeza kasi ya kujikarabati kwa seli za tishu zinazofunika viungo vya ndani ya mwili (epithelial tissue) na ukuaji wa sebum. Ni muhimu kwa ukuaji wa mifupa, meno, watoto na kulinda uwezo wa kuona.

TABIA ZA B-CAROTENE & LICORICE KAMA ANTIOXIDANT.
Kwa kuwa ni mchanganyiko muhimu wa flavonoid, B-Carotene ina tabia za nguvu za antioxidant, inasaidia kupambana na radikali huru na hivyo kupunguza madhara yake kwenye utando unaofunika seli, DNA na protini kwenye seli.licorice ni carotene ng'avu nyekundu inayopatikana ndani ya nyanya na ndani ya matunda na mboga nyingine nyekundu. Umbo la licorice linairuhusu kushambulia radikali huru kirahisi kutoka maeneo yanayoizunguka, na kuifanya kuwa antioxidant ya nguvu.

TABIA ZA KUZUIA KANSA ZA B-CAROTENE & LICORICE.
B-Carotene huzuia zisishambulie DNA kwenye kiini cha seli. Huzuia kusambaa Kwa seli za Kansa hivyo kuzuia Kansa kuhama kutoka sehemu moja hadi nyingine. Ripoti ya kisayansi iliyoandaliwa na mabingwa wa tiba wa Marekani mwaka 1989 inaonyesha kuwa licorice huzuia ukuaji wa saratani ya tezi dume.

KUFANYA DAMU KUWA NYEPESI
Lipids zilizomo ndani ya damu mara nyingi ni triglyceride, cholesterol, phospholipids. Nyingi ya hizi huungana na protini na kujenga lipoprotein ambayo huganywa katika makundi mawili, low density lipoprotein (LDL) na high density lipoprotein (HDL).

Ikiwa kiwango cha LDL katika damu kitakuwa kikubwa, kipenyo cha arteri kitakuwa kidogo, atherosclerosis hutokea na uwezekano wa kupata mshituko wa moyo (heart attack) huwa mkubwa. Hii ndiyo sababu LDL huitwa "bad cholesterol".

Kiwango kikubwa cha HDL hulinda dhidi ya magonjwa ya moyo kwa kutoa LDL nje ya mfumo wa damu. Hii ndiyo sababu HDL huitwa "good cholesterol". B-Carotene na licorice vyote huwasaidia watu wenye umri mkubwa kuzuia kuganda kwa damu na kupunguza uwezekano wa kupata mshituko wa moyo.

Mpendwa msomaji tunashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA, ikiwa unasumbuliwa na tatizo hili au lolote lile iwe wewe au ndugu/jamaa yako msisite kututafuta kwa msaada zaidi wa ushaurI na matibabu PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE KUPITIA KATIKA EMAIL AU NAMBA ZETU ZILIZOPO HAPO JUU KABISA.

KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI ZA AFYA USIKOSE KUTEMBELEA BLOG YETU HII.

Share:

Popular Posts

Blog Archive

for any assistance.

“Your health is your responsibility, love your health as you love your stuff”. -@Paul Biswalo.

We are looking forward to connect with you.

Our phone number is +255 768 603 979,for only calls/text &
+255 ,for WhatsApp only.
Email-address : biswalopaul@gmail.com.

It's me your lovely friend,
Yours in faithfulness,

-@Paul Biswalo, C.E.O & FOUNDER.
Mentor || Motivational Speaker || Trainer || Event Host || Entrepreneur || Healthy & Life coach || Presenter & Inspirational Public Speaker.
*let's meet all at the Top because is no longer crowded*

Featured post

UNAFAHAMU UMUHIMU NA FAIDA YA KUBORESHA KINGA YA MWILI??????

AFYA YAKO NI JUKUMU LAKO. UNAFAHAMU UMUHIMU NA FAIDA YA KUBORESHA KINGA YA MWILI?????? jiulize swali hili na utafakali vizuri ilik...

Followers

Contact Form

Name

Email *

Message *

Labels

Total Pageviews

Theme Support