UHUSIANO KATI YA DAMU NA TABIA
Je unajua kuwa tabia ulizonazo ni kutokana na kundi lako la damu?
Kwa kawaida kila binadamu yuko kwenye kundi mojawapo la damu kati ya
makundi manne A,B,AB na O. Makundi haya yanaweza kutumika kufahamu tabia
za binadamu na jinsi hii yaweza kuwa rahisi na ya karibu zaidi kuliko
kutumia nyota “astrology” kama ambavyo wengi wanafanya, na wataalamu
wanasema tabia kwa uhusiano na kundi la damu ina uhakika zaidi kuliko
wenye vyanzo vingine. Mbali na tabia, ukweli ni kwamba makundi yetu ya
damu yanaweza kutuonyesha pia vile mtu anavyopendelea na asivyopendelea,
kazi anazopendelea, watu anaowapendelea na hata vyakula. Baadhi ya
watafiti nchini korea wamebainisha kuwa hata namna tunavyopendelea
kuketi hutegemea sana na makundi yetu ya damu, sasa tuangalie uhusiano
huu.
ZIFAHAMU GROUP
(MAKUNDI) YA DAMU NA TABIA ZAKE ILI UJINUSURU NA MAGONJWA YAEPUKIKAYO.
Kundi lako la damu linaweza kukufanya uwe dhaifu au imara
katika kukabiliana na magonjwa fulani.Ni vema kujua kundi lako la damu sawa na
ilivyo vema kujua mambo mengine yanayochangia kuwa na afya njema. Kujua kundi
lako la damu Kunaweza kukuza uwezo wako wa kufahamu hatari zinazo kukabili
kutokana na kundi la damu Ulilo nalo na kuepuka hatari hizo kwa kutumia mtindo
wa maisha unaofaa.Hata hivyo, Kama vilivyo viungo vingine vya mwili, damu nayo
ina changamoto ya kukumbana na maradhi mbalimbali, magonjwa yanayoathiri
utendaji kazi wa damu yanaweza kugawanywa katika makundi kama vile ya kurithi,
kuambukiza, mabadiliko ya kimwili na saratani tofauti. Damu ya binadamu imegawanyika
katika makundi makuu manne ambayo ni A, B, AB, na O, binadamu yeyote lazima awe
na moja wapo ya makundi hayo.
Damu kundi “A”(phregmatic).
Hawa watu maranyingi huwa mifano ya kuigwa na wengi kwasababu ya kiu zao na upiganaji wao kwenye mafanikio, ni watu wema,wapole na wenye tabia njema. Pamoja na hayo ni rahisi sana watu hawa kupata msongo wa mawazo “stress” na kufikiria sana vitu. Wakiamua kujitoa kwa ajili ya kumsaidia mtu basi wanazama kabisa na wanaweza hata kujisahau wao.
Mazuri yao
- Ni watu wanaopenda vitu vikamilike katika hali ya juu “perfectionists”, wanapenda mpangilio maalumu, wanapenda na wanaweza kuchambua mambo sawia, wanawajibika na kubeba majukumu yao,wana huruma na wako tayari kusaidia, waaminifu, ni wagunduzi, wanamaanisha, wavumilivu, na wenye tabia njema.
- Wasumbufu,wana hisia kali hata kwenye vitu vya kawaida, wakitaka kitu wametaka, wengine wana aibu,wengine wakimya zaidi na wanaopenda kujichanganya.
- Ni watu Wa gharama sana hasa wadada au wanawake.
- Ni mtu ambaye unaweza kumwamini na kumtegemea
- Anajali na kumaanisha
- Wakati wote huepuka shari,misuguano na magomvi
- Maranyingi hawapendezwi wala kufurahia sherehe zenye makelele na shangwe za ajabu ajabu,wanapendelea ukimya na utulivu.
- Unaweza kumwamini na kumtegemea katika majukumu
- Wanapenda ufanisi wa kiwango cha juu kwahiyo kazi zao mara nyingi ni bora sana.
- Bahati mbaya wanajali sana hata vitu vilivyo vidogo nahii huwafanya kuwa na msongo wa mawazo kirahisi.
- Wasio waelewa vema watu wa kundi hili wanaweza kupata shida kufanya nao kazi.
- Ni waaminifu sana na hapa Mara nyingi unawakuta Maafisa utumishi kwani hufuata sheria.
- Ni ngumu kidogo wao kufunguka na kushirikisha mambo yao.
- sio waongo au wadanganyifu,ni wakweli (they don't like cheating).
- Wanaweza kuonekana wenye aibu, au waoga.
- Ukitaka kumchumbia au kuchumbiwa na mtu wa kundi ‘A’ unahitaji uvumilivu.
- Wakiamua kupenda utawafahamu wakati wote na ingawa watakuruhusu ufahamu tu yale maeneoa ya maishani mwao ambayo wanajua unahusika, hawawi wazi katika kila eneo.
- wanapenda kujifichaficha kama ni usiku hupenda kukaa gizani sana maana wanaaibu sana.
- Ni watu wabunifu na wenye ujuzi wa usanii “artists”
- Wanalewa kirahisi sana, kilevi kidogo tu kitampelekesha sana
- Wengi wao hupendelea kula mboga mboga “vegetarians”
- Hawa ni "vegetarians" wanahitaji sana mananasi na zabibu kwa wingi.
- Watu Wa kundi hili pia huwa wana changamoto ya kuwa na upungufu Wa asidi mwilini hivyo huandamwa na vidonda vya tumbo.
- Ni watu ambao hushambuliwa sana na saratani za mishipa ya fahamu,utumbo,mifuko ya mayai,mfuko wa kizazi na mlango wa uzazi kwa wanawake,kibofu cha mkojo,figo,kongosho na saratani ya kinywa, tezi za mate na umio./kuishiwa na damu mara kwa mara.
- Wana hatari pia ya kupatwa na magonjwa ya Moyo,kupata lehemu mbaya mwilini,kwenye Moyo,wako hatarini pia kupata kiharusi na ugonjwa Wa shinikizo la damu Wa Moyo.
- Vyakula wanavyotakiwa kula kwa wingi ni mbogamboga za Majani na nyama nyeupe nyama nyekundu sio nzuri sana kwa watu hawa.
- hawatakiwi kugusa kabisa au kutumia Mara kwa Mara vyakula hivi :-nyama nyekundu,ngano,,na maziwa.maana vinahitaji asidi nyingi na wao hawana uwezo wa kufanya mmeng`enyo wa vyakula hivi ,kutokana na kuwa na upungufu wa asidi tumboni mwao.
- wakila ndizi,maembe na mapapai huwasababishia waamkapo asubuhi kutokwa na makamasi kwa wingi.
- Wanatakiwa kula kabisa vyakula vyenye asidi kwa wingi kama machungwa,zabibu,passion,malimao,mananasi ,nyanya na jamii yake.
- Watu wa kundi hili wanapenda sana wali na Mara nyingi ndio Chakula chao kikuu.
- Hawatakiwi kugusa kabisa ngano na mahindi na endapo wakatumia vyakula hivi hasa kwa wanawake huwasababishia kupata hedhi Mara mbili kwa mwezi.
Watu wa kundi hili maranyingi ni wenye tabia za kuasi na ni ngumu kuwazuia au kuwatuliza. Wanandoto na maono makubwa,wanasukumwa kwa kasi na kiu zao ingawa wanaweza kuwa wakali na wasumbufu na mara nyingine ngumu kukaa na kuzoeana nao. Wanakisimamia sana kile wanachokiamini hata kama ulimwengu mzima usimame kinyume nao.
- Hili ni kundi la watu ambao ni wazungumzaji yaani ukiwapa nafasi ya kuzungumza ni kama vile umekosea na hapa Mara nyingi unawapata watu kama MCs.
Mazuri yao
Wanasukumwa katika kufikia malengo yao, wako kasi kiutendaji,wanapenda raha,wana hisia nzito , wanayatazama maisha katika mtazamo chanya , wanaweza kujisimamia na kujitegemea na hawahitaji ushirika au kukubaliwa na wengine.
Mapungufu yao
Wabinafsi sana,mara nyingine wanakwepa majukumu yao,wagumu sana kusamehe,wasumbufu,wanaweza kuwa wakatitili na wenye hasira za haraka.
Maisha yao kijamii
Maranyingine ni ngumu kushirikiana nao au kuwa nao maana wanapenda kufanya mambo yao wenyewe.
Kazini
Ingawa wanaweza kuwa na malengo mengi na maono pia lakini wanaweza kuwa wasumbufu na wagumu katika kushirikiana nao kazini. Ni ngumu kufanya nao kazi maana wanataka kufanya pekeyao.
Mahusiano na mapenzi
- Unaweza kufurahi nao sana kwenye mapenzi lakini uwe tayari kuvumilia hasira zao kali na za ghafla. Vumilia hali yao ya kukwepa majukumu pia,fahamu kuwa wanaweza kuwa wakali, wakatili na wasio maanisha kile wanachokisema.
- Wanatabia ya utukutu/umbea kwa sana/wagombanishi na wachonganishi sana.
- Pamoja na baadhi ya mazuri yao bado wanaweza wasiwe watu wazuri kwenye kuwa mume, au kuwa wapenzi wazuri kwa wasichana wao. Hii ni kutokana na urahisi wa tabia za kukosa uaminifu kimapenzi na urahisi wa kuumiza mioyo ya wengine.
- Wanatabia ya kupenda wanyama “they love pets”
- Wana kinga kubwa na imara ya mwili katika kujikinga na magonjwa.
- Wanafurahia zaidi vyakula vitokanavyo na wanyama kama vile maziwa “dairy products” n.k
- Ni watu ambao husumbuliwa sana au wako hatarini kupata magonjwa kama uvimbe Wa fizi,na pia wanawake walioko katika kundi hili wako hatarini kupata ugonjwa Wa kisukari aina ya pili.
- Mara nyingi ni watu ambao wakipata maambukizi ya virusi vya aina yoyote ile huwa machizi au vichaa kutokana na kwamba vinaenda kuharibu mfumo wake Wa fahamu, wana uwezo mkubwa kukabiliana na ugonjwa wa kibindupindu.
- Wana hatari kubwa ya kupata saratani ya koo.
- Watu Wa kundi hili hawashauriwi sana kula vyakula vya aina ya kuku,Karanga,korosho,na nyanya.(Mara nyingi wao wenyewe tu hawapendi kuku ingawa hawaruhusiwi kula),Karanga,korosho,na nyanya.
Kundi hili ni watu wenye haiba mchanganyiko, hawa huwa na tabia tofauti kuanzia kuwa waoga na wenye aibu hadi wengine ni wapenda mitoko na wacheshi,wako wanafanya mambo kwa kuongozwa na mawazo na wengine hawawazi kabisa kile wanacho taka kukifanya,hii inafanya watu wa kundi hili kuwa watu wa kushangaza sana mara unapokuwa nao.
Mazuri yao
- Ni rahisi sana kuwa rafiki nao.
- Wanachukuliana na mazingira haraka na kwa urahisi.
- Wenye kufurahisha unapokuwa nao ingawa ni watu wasiotabirika.
- Wana mawazo,wana akili sana,hupenda kuweka mambo yao kwa vitendo na pia huongozwa na misimamo ya kifikra.
- Wagumu katika kufanya maamuzi.
- Wanasahau sana
- Ni wenye hisia za kayumba “mood swing”, mara wana furaha mara wamekasirika.
- Sio waaminifu.
- Ni wapinzani,wabishi na wakosaji.
- Ni watu wabinafsi.
- Wanaweza kuwa marafiki wazuri na wenye kufurahisha.
- Maongezi yao ni yenye kuhamasisha na yenye akili na kufikiria kwa hali ya juu.
- Kwa kutokuwa wenye kutabirika, wengine huhofia kuumizwa kihisia au kukatishwa tamaa au kuumizwa moyo na watu hawa, hususani pale wanapokuwa sio waaminifu.
- Wanaweza kuwafurahisha na kuwapa burudani mnapofanya kazi nao lakini sio watu wa kuwategemea sana,wanaweza kukuangusha kirahisi.
- Kuwa katika mahusiano na mtu wa kundi la damu la AB kunaweza kuwa kwenye kufurahisha,unaweza usiwe na nyakati nyingi za upweke. Pamoja na haya fahamu kwamba watu hawa wanaweza kuwa wabishi na wakosoaji na maranyingine maneno yao yanaumiza. Mpenzi wa mtu au watu wa hivi lazima aelewe jinsi hisia zao zilivyo na zinavyobadilika mara kwa mara,na pale inapobidi basi uwetayari kuwapa nafasi wanayostahili ili usijiumize sana.
- Ni watu wazuri kwenye mambo yahusuyo fedha.
- Maranyingi wanajihusisha na wanaopendendelea shuhuli za kisanaa au mambo yenye sanaa ‘arts’
- Ni watu wanaoaminika kuwa wabinafsi zaidi hata katika uchangiaji wa damu,watu hawa wanaweza kupewa damu na mtu mwingine yeyote ila wao hawawezi kumpa damu yeyote isipokuwa mwenzao wa AB.
- Kama walivyo watu wa kundi ‘A’ na kundi ‘B’,watu wa kundi la damu ‘AB’ hupendelea vyakula vya mboga mboga “vegetables” na pia vyakula vitokanavyo na wanyama “dairy products”
-
Hawa ni watu ambao Mara nyingi hawaeleweki yaani wana tabia za A na pia tabia za B wakati mwingine.Ni watu ambao wanaweza akaanzisha kitu asikimalizie ukakuta kaishia katikati halafu kaanzisha kingine.KIAFYA ZAIDI.✔Ni watu ambao wako hatarini Kupata magonjwa kama kiharusi,dengue,magonjwa ya Moyo,shinikizo la Moyo,na lehemu kujaa kwenye mishipa ya damu.✔Watu Wa kundi hili Mara nyingi wakifikia uzeeni uwezo wao Wa kufikiri hupungua kwa haraka.Lakini Mara nyingi kupungua kwa uwezo Wa kufikiri hutokana na magonjwa kama shinikizo la Moyo,kisukari na lehemu kuwa nyingi sana mwilini.✔ ni watu ambao wana uwezo mkubwa sana Wa kukabiliana na magonjwa yaani kinga yao ya mwili ni imara ukifananisha na makundi mengine yote ya damu.
Hawa maranyingi wanajitahidi kuwa mahodari na mashujaa katika mambo tofauti. Mara zote kiu yao ni kuwafurahisha na kuwapendeza watu wengine ni wenye moyo wa uongozi wenye kiu ya kuwaona rafiki zao wakiwa wenye furaha wakati wote. Sio wagumu wa mabadiliko, wako tayari kubadilika, ni wenye mawazo mapana naya wazi, sio wagumu kifikra na ni marafiki wazuri.
Faida zao
- Ni wenye ujasiri, wanashindana katika mambo mengi mfano mambo ya maendeleo, hufanya kazi sana na kwa bidi, ni waaminifu, wanaweza kujieleza, ni marafiki wazuri, wanasamehe, mitazamo yao ni chanya, huweza kuhisi au kuonamambo hata kabla hayajatokea,wanakiu ya kufahamu na kudadisi na pia niwatu wema na watoaji.
- Maranyingine wanaweza kuwa wenye fujo, wanaopenda sifa, wanavutia vitu upande wao, wanaepuka au kukwepa majukumu,unaweza kuona hawa wanaigiza mambo, wakitaka wametaka hadi wapate na nirahisi kuwaondoa kwenye kile wanachokifanya “easy to be distracted”.
- Hawa ni watu ambao ni jeuri na kiburi na wanajiamini sana. watu ambao ni wababe,wagumu,wenye ubinafsi na wanafanya maamuzi yao pale wanapoamua na sio kulazimishwa.
- Ni marafiki wazuri na unaoweza kuwategemea, ni waaminifu, ni wawazi,ingawa mara nyingine wanaweza kukuudhi, pia wakati mwingine wanatamani kusikilizwa wao tu.
- Wana kiu ya mafanikio, hufanya kazi kwa bidii ingawa kukatishwa tama na kupoteza hamasa ya kazi kirahisi sana. Mara nyingine ili wafikie malengo ni vema wakisimamiwa kwenye kazi wanayo fanya badala ya kuachwa wafanye wenyewe.
- Ni watu wanaoweza kuonyesha mapenzi kwa wale wanaowapenda ila ni vema ukafahamu kuwa watu hawa hutarajia upendo wa jinsi ile ile wao wanavyoonyesha upendo kwako bila hivyo utakosana nao.
- Wanaaminika huwa na tabia za kijeshi.
- Wengi wao kwa asili ni watu wa kupenda michezo.
- Wanaaminika kuwa watu wema na waliotayari kusaidia mtu yeyote, hata katika uchangiaji wa damu ‘watu wa kundi ‘O’, wanaweza kumpa damu mtu mwingine yeyote.
- Wanapendelea na kujisikia raha wanapokula nyama “meet lovers”.
- watu ambao wana roho nzuri sana ila hawapendi uongo hivyo usije ukajaribu kuwadanganya hata siku moja.
KIAFYA ZAIDI.
✔ Ni Watu ambao sio rahisi sana
kupata shambulio la ghafla la Moyo kama ilivyo kwa watu wenye makundi mengine
ya damu.
✔ Hawana kinga ya kutosha dhidi
ya kipindupindu lakini wana kiasi fulani cha kinga dhidi ya Kifua Kikuu (TB),
Malaria isiyo kali, saratani za kongosho, tumbo, matiti na mlango wa kizazi.
✔Ni rahisi kupata magonjwa ya
maambukizi ya ngozi,na vidonda vya tumbo.Wanapata sana maumivu ya kiuno,magoti
pamoja na mgongo.
✔Ni watu wasiopenda vitu
vichachu kutokana na uwepo Wa asidi kwa wingi mwilini mwao hivyo wanasumbuliwa
sana na vidonda vya tumbo na huwa wanasumbuliwa sana na tatizo la choo
(constipation) pamoja na kisukari.
✔Kundi hili pia hutokewa na mvi
za mapema sana.
✔Kwa wanaume hapa ndipo
unawakuta ambao wana mapaja yasiyolingana yaani moja kubwa lingine Dogo.
HAWATAKIWI KUFANYA YAFUATAYO.
✔Hawatakiwi kula ngano na
mahindi Mara kwa Mara au kutokula kabisa.
✔ Hawapaswi kabisa kugusa au
kula machungwa,passions,ukwaju,maembe mabichi n.k na vyote vyenye asidi.
✔Hawatakiwi kabisa kula ugali au
wali,mahindi ya kuchoma au kukaanga au kupika hayawafai kabisa.
✔Wanaume walioko katika kundi
hili wanahitaji protini kwa wingi kuliko wanawake kutokana na kuhitaji nguvu
kwa sana katika shughuli zao na miili yao kwa ujumla.
✔Kwa wanaume wanatakiwa kula
matunda sana kama papai,mananasi,ndizi,matikiti maji (ule na mbegu zake) hapa
pia kama ni tunda unakula lote mfano nanasi unalimaliza,papai unalimaliza,na
pia matunda ya rangi moja kula kwa pamoja.
✔Ukitengeneza kitu kama juice ya
matunda unywe yote kwa wakati huo na sio kutengeneza ya wiki au siku kadhaa.
✔ wanapenda sana kula nyama yenyewe hasa
ya mbuzi na ya ng'ombe ya kuchoma.
✔Vyakula vinavyowasaidia au
wanavyohitaji sana mwilini ni matunda ,mboga za Majani,protini kwa wingi yaani
nyama,maharage,mayai na maziwa.
NB:Magonjwa mengi yanaweza kuepukwa kwa kuzingatia usafi wa
mwili na mazingira, mlo kamili(kula kilingana na Uhitaji wa group/kundi lako la
damu), kufanya mazoezi, kupunguza uzito uliozidi na kuepuka matumizi ya
tumbaku, pombe pamoja na dawa za kulevya.
kwa mawasiliano zaidi: +255768603979“ maamuzi yako ya sasa ni matokeo ya baadaye”.
fuatilia taarifa zaidi kupitia hapa:
https://web.facebook.com/Yourhealthyourprioritylifestyles/…
https://paulbiswalo.blogspot.com/
https://web.facebook.com/MaishaNiAfyaLindaAfyaYako/
https://www.pinterest.com/biswalopaul/
SHARE NA UNAOWAPENDA ILI WAFAIDI ELIMU HII YA BURE.
KWA KUENDELEA KUPATA UP-DATE JUU YA AFYA LIKE PAGE HII NA KUSHARE
ELIMU HII YA BURE KWA WENGINE.
No comments:
Post a Comment
warmly welcome
contact us via +255 768 603 979.