Health And Wellness Is Your Priority & Personal Development Mentorship Programs.

“Your health is your responsibility, love your health as you love your stuff”. -@Paul Biswalo.

We are looking forward to connect with you.

Our phone number is +255 768 603 979,for only calls/text &
+255 ,for WhatsApp only.
Email-address : biswalopaul@gmail.com.

It's me your lovely friend,
Yours in faithfulness,

-@Paul Biswalo, C.E.O & FOUNDER.
Mentor || Motivational Speaker || Trainer || Event Host || Entrepreneur || Healthy & Life coach || Presenter & Inspirational Public Speaker.
*let's meet all at the Top because is no longer crowded*
HUU NI UKAUZU KWA KWELI....KAMA NI WEWE UNGEFANYAJE??


Baada ya miaka minne ya kuajiriwa bila hata kuongezwa mshahara au hata marupurupu, Bwana Saadaty Hassani aliamua kwenda kwa bosi wake kulalamika.


Jibu alilolipata kwa bosi wake ni kwamba hakupewa nyongeza wala marupurupu kwa sababu HAKUSTAHILI.


Akauliza kwa nini?


Akaambiwa katika miaka minne uliyofanya hapa, hujafikisha mwaka hata mmoja.


Akasimama na kuanza kufoka, akaambiwa kaa chini, na majibizano yakawa hivi;


Bosi; Mwaka una siku ngapi?


Saadaty: 365 au 366.


Bosi: Huwa unakuja kazini wikiendi?


Saadaty: Hapana


Bosi: Hebu piga hesabu mwaka una jumamosi na jumapili ngapi kisha zitoe katika 366


Saadaty: Jumamosi 52 na Jumapili 52 jumla unapata siku 104. Ukitoa katika siku 366 unabaki na siku 262.


Bosi: Siku ina masaa 24, wewe unafanya kazi masaa mangapi?


Saadaty: Masaa nane kwa siku


Bosi: Sasa nipigie hesabu masaa nane katika masaa 24. Nane kwa 24 inaingia mara ngapi?


Saadaty: Inaingia mara tatu mkuu


Bosi: Sasa ukizigawa zile siku 262 kwa masaa uliyofanya kazi yaani uigawe kwa tatu kulingana na masaa uliyofanya kazi unapata siku ngapi zilizokamilika?


Saadaty: 87


Bosi; Kwa mujibu wa saa ulizofanya kazi kwangu, ni sawa na siku 87, tuendelee na mahesabu?


Saadaty: Tuendelee


Bosi: Unakumbuka uliumwa wiki mbili nikakupa likizo? Na ulishachukua likizo yako ya kawaida siku 28 na ukaenda msibani wiki moja hebu piga hesabu vizuri.


Saadaty: 14 + 28 + 7 = 49


Bosi; Toa katika siku 87


Saadaty: 42


Bosi; Toa sikukuu za Idd, Maulid, Uhuru, Mapinduzi, Pasaka, Krismas, Nyerere Day, Mwaka mpya, Mei Mosi, Sabasaba, Nanenane na ile wiki iliyonyesha mvua kuuubwa nikawaruhusu mpumzike.


Saadaty: Bosi naomba nikaendelee na kazi


Bosi: Malalamiko vipi?


Kuwa bosi wako mwenyewe....


Fanya kazi kwa muda na masaa unayotaka wewe...


Amka muda unaotaka wewe baada ya usingizi kuisha sio muda unaolazimika kwa sababu uzijuavyo....


Tumia muda wako vizuri.....masaa 8 fanya kazi,8 mengine ni ya kupumzika nikimaanisha kulala na yaliyobakia fanya kitu ambacho kitakuzalishia au kukuletea kipato endelevu......


mtegemea cha bosi pekee hufa masikini wakati wengine wanatambua fursa mbalimbali wanzaokutana nazo na kuzifanyia kazi wanafanikiwa sana kufikia mahali wanapohitaji kuwa na majina yao yanabadirika ,mfano wao ni akina REGINALD MENGI,SAALIM BAKHRESA,MOHAMED DEWJI ,MILLARD AYO,ERICK SHIGONGO,PAUL BISWALO na wengine wengi hapa tanzania.


*........KAMA WEWE UPO HIVYO BADILIKA.............
HUU NI WAKATI WA KUWAFUNDISHA WATU UKWELI ILI WAPATE KUFANIKIWA PASIPO KUTEGEMEA AJIRA PEKEE ETI ZITAWAFANIKISHA WAKATI UKWELI NI KWAMBA AJIRA NI MTEGO WA KUFANIKIWA KATIKA MAISHA YA WAJIRIWA NA KUSHINDWA KUISHI NDOTO ZAO MAANA ZINAWABWETESHA AKILI NA KUZIFANYA KUWA MGANO NA KUISHI MAISHA YA KIMASIKINI KABISA. e.t.c.........................................*


Umaskini sio hali ya kukosa mali na kuwa na hali duni, umasikini ni mtazamo usioweza kuzalisha, usiowaza kufanikiwa, usiotaka kujituma.


Ebu pokea hili wazo la utajiri upate kufanikiwa, na wewe uliyefanikiwa acha kuwaza kimaskini.


Yupo maskini mwenye mawazo ya utajiri, na yupo tajiri mwenye mawazo ya kimaskini tumia utajiri wako kwa ajiri ya kazi ya BWANA.




ZIFUATAZO NI SIRI SITA AMBAZO MWAJIRIWA HAZIFAHAMU ZINAZOWAFANYA WASIISHI NDOTO ZAO NA BADALA YAKE WANAISHI NDOTO ZA BOSI WAKE.


1)kuanza safari ya maisha bila kuwa na ramani ya uendako.
2)kuwaza pesa kuliko kuwaza wazo la kukuingizia pesa,hapa mtu yuko tayari kuajiriwa alipwe kiasi kidogo tu cha pesa mwisho wa mwezi kuliko kufanya shughuli zake mwenyewe kisa eti mshahara upo kila mwezi na akifanya mambo yake binafsi hayamhakikishii kupata pesa katika maisha yake kwa wakati.
3)kutokujua kuwa kipato chako kinategemeana na thamani au mchango wako sokoni.wakati ukiangalia pesa unayolipwa haiendani kabisa na elimu yako na ujuzi wako.
4)ukosefu wa mpango endelevu wa kurithisha kizazi baada ya kizazi,hapa unamkuta mtu anaringa na cheo chake utafikiri atamuachia mwanae wakati hatima ya maisha yake yako kwa bosi na akifukuzwa hana kitu hata watoto wake pia watajitafutia kila kitu mpaka kuja kufikia cheo kama cha mzazi wake.
5)kufikiri kunakoongozwa na hofu badala ya ndoto,anahofia kufukuzwa kazi tu muda wote anaacha kuwaza ndoto zake maana pia ukitazama pesa anayopata ni ndogo sana kulinganisha na muda aliowekeza kwa bosi na sio kwa mambo yake binafsi.
6)kukosa uelewa wa ujengaji utajiri wa ukweli ,hapa utakuta mtu anaamua kujilimbikizia mali eti kisa rafiki yake kafanikiwa yeye hakuna ,utamkuta anakula rushwaili aje kuwa tajiri mwisho wa siku anaishia jela.

Haya ndio wajiriwa wengi hawajui ,wanaishia kuringi cheo chake ,nikwambie tu cheo ni dhamana na pia nikama nguo ya kuazima mwenye nayo akija anahitaji nguo yake haijalishi umekutananaye maeneo gani,utaumbuka akianza kukuvua nguo yake na ukweli watu wataufahamu ukiwa uchi kama ulivyozaliwa baada ya nguo kuchukuliwa na mwenye nao.

Tafuta kitu cha ziada ufanye kwa muda wako wa ziada,na kama hujui nini cha kufanya wasiliana na mimi nitakusaidia ufanye nini ili uishi maisha ya ndoto zako kwa kupitia namba hii +255768603979.

" Change your MIND, before you change your LIFE ".
*YOU ARE WHO YOU ARE BECAUSE OF YOUR MIND*..!
Jipatie nakala yako ya #BE EMPLOYED WITH PLAN "B",unaweza kuweka oda yako mapema kupitia namba hii +255768603979,ili uepukane na mawazo mgando yakulalamika bila kufikia ndoto zako wakati wengine wanaopenda kusoma vitabu wanapata mawazo na mbinu mpya za kufanikiwa na maisha yanakwenda vizuri.


wako katika kuijenga imani yako juu ya kufanikiwa katika jambo unalohitaji katika maisha yako,
-Paul Biswalo.
Mhamasishaji,Muelimishaji,Mkufunzi,Mwalimu.
(Mwenye Vipaji Vingi/Asiyekuwa na Kikomo).


#Badilika#
#Shtuka#
#Amka#


#HapaKaziTu.








Share:
KAMA WEWE NI MPENZI WA KUSOMA VITABU TAFADHALI JIFUNZE KITU HAPA

UNAHITAJI KITABU ZAIDI YA UNAVYOWEZA KUDHANI.
�〰�〰�〰�
©Habel Samida:
Mwandishi na Mhamasishaji.

Umeshafanikiwa kuandika kitabu? Kama umefanikiwa HONGERA SANA. Kama bado, umeshawahi kuwaza kuandika?

Ukweli ni kwamba, unahitaji sana kuandika kitabu. Unaweza kujiuliza "kwanini niandike kitabu? Naanzaje?" Majibu yote yako hapa.

Nilieleza hapo awali kwamba, unahitaji sana kuandika kitabu zaidi ya vile unavyoweza kufikiria. Zifuatazo ni baadhi ya sababu; kwanini uandike kitabu.

1. Una kitu ambacho wengine wanatamani kukifahamu.

2. Kitabu kitaendelea "kuishi" hata wewe usipokuwepo juu ya uso wa dunia. (Kitaacha alama zako)

3. Utaaminika na kuchukuliwa kama mtu uliyebobea au naweza kusema "professional".
Nimejifunza kwamba, unapokuwa umeandika kitabu, mtazamo wa watu juu yako hubadilika. Thamani yako huongezeka, kwakuwa umethubutu kufanya jambo ambalo asilimia ndogo sana ya watu duniani huwa na ujasiri wa kulifanya.
Licha ya hivyo, utaaminika zaidi, ukizingatia kuwa; watu wanaamini sana katika kile wanachokisoma kuliko kusikia! Kwa mfano; kama unasimulia ajali iliyotokea mahali Fulani, ambapo uliishuhudia halafu akaja mtu mwingine akaanza kukubishia kwamba haikuwa hivyo! Akatoa gazeti ambalo limeripoti habari hiyo.
Kiuhalisia mtu huyo atakuwa sahihi kwakuwa ana ushahidi. Hata kama mwandishi aliyeripoti habari hiyo hakuwepo kushuhudia tukio.
Ni kwa sababu, watu wanaamini sana katika kile wanachokisoma.

4. Kitabu kitafungua milango mingi ambayo hukutegemea.
Hii ni mbinu aliyonifundisha mwalimu wangu Rene katika tasnia ya uhamasishaji. Alianza kuandika kitabu akiwa ameajiriwa kama mfagizi katika hoteli. Baada ya kuandika kitabu chake, kilifungua milango mingi sana. Aliitwa kwenye vituo vya redio na televisheni mbali mbali na kupata mialiko kuongea katika mikutano mbalimbali.
Hapo maisha yake hayakubaki vile yalivyokua.
Nimeshuhudia kwangu pia, nilipofanikiwa kuandika kitabu cha JAHILI, kilinifanya nikutane na watu ambao sikutarajia.

POWERED BY:http://paulbiswalo.blogspot.com/
 
 
 
Share:

Popular Posts

Blog Archive

for any assistance.

“Your health is your responsibility, love your health as you love your stuff”. -@Paul Biswalo.

We are looking forward to connect with you.

Our phone number is +255 768 603 979,for only calls/text &
+255 ,for WhatsApp only.
Email-address : biswalopaul@gmail.com.

It's me your lovely friend,
Yours in faithfulness,

-@Paul Biswalo, C.E.O & FOUNDER.
Mentor || Motivational Speaker || Trainer || Event Host || Entrepreneur || Healthy & Life coach || Presenter & Inspirational Public Speaker.
*let's meet all at the Top because is no longer crowded*

Featured post

UNAFAHAMU UMUHIMU NA FAIDA YA KUBORESHA KINGA YA MWILI??????

AFYA YAKO NI JUKUMU LAKO. UNAFAHAMU UMUHIMU NA FAIDA YA KUBORESHA KINGA YA MWILI?????? jiulize swali hili na utafakali vizuri ilik...

Followers

Contact Form

Name

Email *

Message *

Labels

Total Pageviews

Theme Support