Uvimbe
Kwenye Mayai ya Mwanamke (Ovarian Cyst)
mayai ya mwanamke (ovary) hutokana
na mkusanyiko wa majimaji yanaozungukwa na kuta nyembamba ndani ya mayai ya
mwanamke. Uvimbe huu ambao hupatikana ndani ya mayai ya mwanamke ndio
unaojulikana kama ovarian cyst.
Uvimbe huu hutokea kwa wanawake wa
umri wowote ule na mara nyingi huonekana kwa wanawake waliokatika umri wa
kushika ujauzito.
Lazima nikiri ya kwamba shauku ya
kuandika makala hii inatokana na swali la msomaji wetu mmoja alilouliza
“Nimepiga ultra sound nikaambiwa nina kitu cheupe kwenye ovari yangu moja je
hili tatizo linaweza kunifanya nisishike mimba? na matibabu yake yakoje? na pia
naumwa sana nyonga tiba yake ni nini. Nitashukuru kwa msaada wako.” Mwisho wa
kunukuu.
Sina nia ya kusema ya kwamba tatizo
lake ni hili la uvimbe katika mayai ya mwanamke, la hasha, kwa sababu
sijaiona ultrasound yake na historia yake aliyotoa msomaji huyu ilikuwa
haijitoshelezi. Hivyo, nina imani ya kuwa kwa kupitia makala hii yeye pamoja na
wasomaji wengine wanaweza kupata mwanga juu ya tatizo hili la uvimbe katika
mayai ya mwanamke.
Mayai
ya mwanamke ni nini?
Kwa kawaida mwanamke anakuwa na mayai mawili
katika mwili wake. Yai moja upande wa kulia na yai jingine upande wa kushoto
kwake. Mayai haya hupatikana pembezoni mwa mfuko wa uzazi (uterus). Mayai haya
ya mwanamke huanza kuzalisha mayai ya uzazi yanayojulikana
Mayai haya ya uzazi huishi kwa masaa
machache hadi masaa 24 bila kurutubishwa na mbegu za kiume kutoka kwa
mwanamume. Mabaki ya mfuko wa mayai ya uzazi yanayojulikana kama follicle ndani
ya ovari, hugeuka na kuwa corpus luteum
ambazo huusika na utoaji kichocheo aina ya progesterone
kwa wingi. Ni kichocheo hiki cha progesterone
ndicho husababisha mfuko wa uzazi kujiandaa kwa upachikwaji (implantation) wa yai lililorutubishwa
kwa mbegu ya kiume ndani ya mfuko wa uzazi kwa kuongeza unene kwenye kuta zake.
Yai hili husafiri hadi kwenye mfuko
wa uzazi kwa ajili ya kwenda kujipachika. Kama upachikwaji wa yai
lililorutubishwa kwa mbegu za kiume (au kama yai la uzazi ambalo
halijarutubishwa) hautafanyika, basi ndani ya wiki mbili, corpus luteum huanza kusinyaa na kupotea yenyewe (involute) na
kusababisha kushuka kwa kiwango cha vichocheo aina ya progesterone na estrogen.
Kushuka kwa viwango vya vichocheo
hivi husababisha mfuko wa uzazi kuanza kutoa mabaki ya kuta zake pamoja na yai
la uzazi na hii ndiyo pale mwanamke hupata damu za hedhi (menstruation).
Unaweza ukajiuliza, ni kwa nini mwandishi ameanza na maelezo ya hedhi? Hapa
nilitaka kuonyesha umuhimu wa mayai ya uzazi kwa mwanamke pamoja na kazi yake.
Kuna
aina ngapi za uvimbe kwenye mayai ya mwanamke?
Kuna aina nyingi za uvimbe kwenye
mayai ya mwanamke lakini aina hizi saba ndio huonekana sana kwa wanawake wengi
ambazo ni;
- Follicular cyst - Hutokea wakati ovulation isipotokea au baada ya corpus luteum kuanza kusinyaa na kupotea yenyewe baada ya kutokupachikwa kwa yai kwenye kuta za mfuko wa kizazi. Uvimbe huu unakuwa na wastani wa 2.3 inches kwa upana. Upasukaji wa uvimbe huu husababisha maumivu makali sana katikati ya mzunguko wa hedhi yaani siku ya ovulation. Maumivu haya yanayojulikana kama mittelschmerz huonekana kwa wanawake robo moja wenye aina hii ya uvimbe. Kwa kawaida, uvimbe huu hauna dalili zozote na hupotea wenyewe baada ya miezi kadhaa.
- Corpus Luteum cyst - Kutokana na kutopachikwa kwa yai la uzazi lililorutubishwa na mbegu ya kiume kwenye mfuko wa kizazi, corpus luteum husinyaa na kupotea yenyewe, aghalabu inaweza kutokea corpus luteum ikajaa maji na hivyo kusababisha uvimbe wa aina hii. Kwa kawaida, uvimbe huu huonekana kwenye upande mmoja (kushoto au kulia) wa mwanamke na hauna dalili zozote zile.
- Hemorrhagic cyst - Uvimbe huu hutokea wakati kukiwa na uvujaji wa damu ndani ya uvimbe wa aina yoyote ule ambao umeshajitengeneza tayari. Huambatana na maumivu makali kwenye upande mmoja wa ubavu wa mwanamke (kushoto au kulia).
- Dermoid cyst - Uvimbe huu ambao sio saratani na pia hujulikana kama mature cystic teratoma, huathiri wanawake wadogo walio katika umri wa kushika mimba na huweza kukua na kufikia inchi 6 kwa upana na ndani yake huweza kuwa na mchanganyiko wa nywele, mfupa, mafuta na cartilage. Uvimbe wa aina hii huweza kuwa mkubwa zaidi (inflamed) au kujizungusha (torsion) na hivyo kuathiri usambazi wa damu kwenda kwenye uvimbe huu na hivyo kusababisha maumivu makali sana maeneo ya tumboni.
- Polycysitic appearing cyst - Uvimbe wa aina hii unakuwa ni mkubwa sana na huwa umezungukwa na vijivimbe vyengine vidogo vidogo na huonekana hata kwa wanawake wenye afya njema au wale wenye matatizo ya homoni.
- Cystedenoma - Ni aina ya uvimbe unaotokana kwenye tishu za ovary na hujazwa na majimaji aina ya kamasi.Uvimbe wa aina hii huweza kuwa mkubwa sana hata kufikia inchi 12 au zaidi kwa upana.
- Endometriomas /Endometrial Cysts - Husababishwa na uwepo wa aina mojawapo ya kuta za mfuko wa kizazi unaojulikana kama endometrium kwenye mayai ya mwanamke (ovary). Huathiri wanawake waliokatika umri wa kushika ujauzito na huambatana na maumivu sugu ya nyonga (chronic pelvic pain) wakati wa hedhi. Uvimbe huu unakuwa na damu ya rangi ya nyekundu kahawia (reddish brown) na ukubwa wake ni kuanzia 0.75-8 inches.
Nini
husababisha tatizo hili la uvimbe kwenye mayai ya mwanamke?
Vihatarishi vya tatizo hili ni
- Historia ya awali ya ovarian cyst.
- Kuwa na mzunguko wa hedhi usiotabirika (irregular menstruation cycle)
- Kuwa na mafuta mengi kwenye sehemu ya juu ya mwili (kwa wale wanawake wanene)
- Ugumba
- Kuvunja ungo/Kubalehe mapema ( kuvunja ungo ukiwa na miaka 11 au chini yake)
- Kukosekana kwa uwiano sawa wa vichocheo mwilini au ugonjwa wa aina ya hypothyroidism.
- Tamoxifen – Dawa ya kutibu saratani ya matiti.Hii ni moja ya madhara ya dawa hii.
I. Mvurugiko wa homoni za mwanamke ni kitendo cha kuongezeka au kupungua kwa vichochezi katika mwili wa mwanamke pale anapo pata hedhi, hivyo
kufanya mwili
kubadilika.
Mvurugiko huo
huathiri kila mwanamke kwa zaidi ya 80%.
Asilimia
kubwa ya wanawake mabadiliko
huanza kati ya miaka 40 na 50,
lakini pia kukosekana kwa usawa wa homoni huweza kuonekana mapema zaidi, kuanzia
miaka 14.
Mabadiliko
haya
asilia hutokea wakati wa balehe,
hedhi, ujauzito, kabla na baada ya ukomo wa hedhi. Mvurugiko wa homini kwa mwanamke huweza
kuchangiwa kutokuwepo na usawa katika homoni zifuatazo Estrogen,
Progesterone na Testosterone. Kupungua au kuzidi kwa homoni hizi
kupelekea mvurugiko
wa homoni
kwa mwanamke.
II. VYANZO VYA MVURUGIKO WA HOMONI
Mvurugiko wa homoni ni tatizo
linalowakumba wanawake wengi kwa sasa, hii ni
kutokana na maisha wanayoishi,
elimu finyu waliyonayo
juu ya afya zao na kutokula
kulingana na makundi ya damu.
Vyanzo vya kuvurugika kwa homoni
ni:
-Uwepo wa sumu mwilini
-Unbalanced Lifestyle (mfumo
mbovu wa maisha)
-Umri ukienda sana
-Kukoma kwa hedhi
-Kutofanya mazoezi,
na kutokulala masaa anayostahili kwa siku
-Uzito mkubwa
-Mabadiliko ya mazingira au hali ya hewa
-Msongo wa mawazo
-Kula vyakula visivyo
endana na Blood Group
-Upungufu wa lishe mwilini
-Matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango
-Utoaji wa mimba
-Family History (Upungufu au ongezeko ya homoni ya progesterone na Estrogen)
-Ongezeko
ya homoni ya Androgen (Kuota ndevu,
sauti kama mwanaume)
-Bara (Ethnicity): Wanawake wa Afrika wengi wana hili tatizo la ongezeko
ya Homoni ya Estrogen,
ndiyo
maana wana maumbile makubwa.
Dalili
na viashiria
- Maumivu makali, ambayo hayana mwanzo maalum, yanayochoma, maumivu haya yanaweza yakawa yanakuja na kupotea au yakawepo moja kwa moja. Pia mtu anaweza kupata usumbufu (discomfort) kwenye maeneo ya chini ya kitovu, kwenye nyonga, uke (vagina), kwenye mapaja na mgongoni kwa chini.
- Kuhisi tumbo kuwa zito, limejaa au limevimba.
- Maumivu kwenye matiti
- Hedhi isiyotabirika
- Maumivu ya muda mrefu kwenye nyonga wakati wa hedhi na ambayo huweza kuhisiwa sehemu ya chini mgongoni.Maumivu haya yanaweza kuanza muda mfupi tu baada ya kuanza hedhi, wakati wa hedhi au mwisho wa hedhi.
- Maumivu ya nyonga baada ya kufanya kazi ngumu/mazoezi au baada ya kufanya mapenzi/kujamiana.
- Kichefuchefu
- Kutapika
- Kutokwa na matone ya damu kwenye tupu ya mwanamke au kutokwa na damu kupitia ukeni.
- Ugumba.
- Uchovu
- Mabadiliko ya haja ndogo-Kukojoa mara kwa mara, au kujikojolea, au kushindwa kutoa mkojo wote kutoka kwenye kibofu cha mkojo wakati wa kupata haja ndogo.
- Mabadiliko ya haja kubwa-Kupata haja kubwa kwa shida sana kutokana na presha kwenye maeneo ya nyonga.
- Nywele kuwa kubwa sana
- Kuongezeka kuota kwa nywele kwenye uso au sehemu nyingine za mwili
- Kuumwa kichwa
- Kuongezeka uzito
- Maumivu ya kwenye mbavu
- Kufanya uvimbe chini ya ngozi
- Kuvimbiwa (bloating)
Vipimo
vya uchunguzi
•
Endovaginal Ultrasound - Ultrasound inayofanywa kwa kuingiza mpira maalum
kupitia ukeni/tupu ya mwanamke na kuangalia mfuko wa uzazi na mayai ya
mwanamke. Kwa kutumia kipimo hiki, ni rahisi kwa daktari kugundua kama uvimbe
kwenye mayai ni wa aina gani kama ni maji tu (fluid filled
sac), complex (maji pamoja na mchanganyiko wa vitu vigumu), au ni vitu vigumu pekee
(completely solid).
• Abdominal
Pelvic Ultrasound - Ultrasound ya kawaida. Husaidia kujua ni aina gani ya
uvimbe uliopo kwenye mayai ya mwanamke. Mara nyingi, uvimbe kwenye mayai
ya mwanamke huonekana kama maputo (bubbles).
• CT Scan
• MRI
• Serum
CA-125 Assay - Kipimo cha damu kuangalia kiashiria cha CA-125 (Cancer Antigen
125). Kupatikana kwa kiashiria hiki huonyesha ya kwamba mwanamke ana saratani
ya mayai ya mwanamke aina ya Epithelial Ovarian Cancer. Pia huweza kuonekana
kwenye magonjwa mengine ambayo siyo saratani kama endometriosis, uterine
fibroids nk.
• Urine for
pregnancy test - Kipimo cha kuangalia ujauzito kwani matibabu ya uvimbe kwenye
mayai hutofautiana kwa mwanamke mwenye ujauzito na yule ambaye hana ujauzito. Pia
husaidia kujua kama mwanamke ana mimba iliyotunga nje ya mfuko wa kizazi
(ectopic pregnancy) au la, kwani uvimbe kwenye mayai ya mwanamke huweza
kuonyesha dalili zinzoshahabiana na dalili za mimba iliyotunga nje ya
mfuko wa kizazi.
•
Culdocentesis - Kipimo kinachofanywa kwa kuchukua maji kutoka katika mfuko
unaojulikana kama pouch of douglas ulio katikati ya puru (rectum) na
shingo ya kizazi ili kuangalia kama kuna maambukizi katika uke (Pelvic
Inflammatory Disease) au mgonjwa ana mimba iliyotunga nje ya mfuko wa uzazi.
• Hormone
levels - Kuangalia kiwango cha vichocheo aina ya Luteinizing Hormone, Follicle
Stimulating Hormone, Testosterone, Estardiol na nk.
• Complete
Blood Count - Kipimo cha kuangalia wingi wa damu na seli tofauti za damu.
• Doppler
Flow Studies.
Tiba
ya uvimbe kwenye mayai ya mwanamke
Tiba ya Dawa.
Tiba hii huusisha matumizi ya dawa
za upangaji uzazi (oral contraceptives)
kwa muda wa wiki 4-6. Matumizi ya dawa hizi kwa muda mrefu huzuia kutokea tena
kwa uvimbe kwenye mayai ya mwanamke lakini zina madhara makubwa sana
kiafya,ingawa huwa hawapendi kuwambia ukweli pindi wanapokushauri kutumia
wanaishia kusema tu ,utapata maudhi madogo madogo ambayo ni ya kawaida na wewe
unakubali mwisho wa siku unaenda siku zako mwezi mfululizo hapo ndio unaanza
kupata shida nyingine. Dawa hizi hufanya kazi kwa kuzuia mayai ya mwanamke
(ovary) kutoa mayai ya uzazi (ovums). Aidha, dawa hizi hazipunguzi uvimbe huu
kwani uvimbe hupotea wenyewe, baada ya muda UVIMBE unarudi tena. Dawa za
maumivu hutolewa kwa wale wenye kupata maumivu makali sana. Matumizi ya dawa za
matatizo ya uzazi (fertility drugs)
husababisha tatizo la ovarian hyperstimulation
ambalo huambatana na uvimbe kwenye mayai ya mwanamke, uvimbe wa aina hii
hupotea baada ya mwanamke kupata hedhi au baada ya kujifungua lakini haikuhakikishii kuwa uvimbe/tatizo
hili ndio umeondoka moja kwa moja mwilini mwako.
ANGALIZO.
Wanawake wengi baada ya kujifahamu/kujigundua kuwa homoni zao haziko sawa huenda
mahospitalini ambako hupewa madawa
yenye kemikali (bioidentical or synthetic hormones)
na wengine hufanyiwa hormone replacement therapy.Tiba hii huandaliwa kwa ajili ya kuzifanya homoni zifanye kazi zake kama kawaida ila bila kuondoa tatizo kabisa. Lakini hupelekea madhara yaliyotajwa hapo awali (juu) bila
kufahamu madhara yake maana ndio Suluhisho Linalopendwa sana na wanawake wa karne hii.mwisho
wa siku wanajikuta wamejitumbukiza kwenye janga kubwa na zito ambalo mwisho wa
siku ilisipopona hupelekea kuharibu kizazi na kupelekea kukosa watoto na kuanza
kusingizia uchawi kumbe mchawi ni yeye mwenyewe.
Tiba ya Upasuaji.
Exploratory Laparatomy - Mgonjwa
hupasuliwa kwenye maeneo ya tumboni ili daktari aweze kuondoa uvimbe uliopo
ndani. Upasuaji hufanyika kwa wanawake wenye;
• Uvimbe
ambao unajulikana kama complex ovarian cyst na ambao haupotei wenyewe
• Uvimbe
unaosababisha dalili na viashiria nilivyotaja hapo awali na ambao pia haupotei
wenyewe
• Uvimbe
mkubwa kuanzia 5cm-10cm na
• Wanawake
ambao wamefikisha umri wa kutopata hedhi tena au wanakaribia umri huo
(miaka 42-58).
Laparascopic Surgery - Upasuaji
unaofanywa kwa daktari kupasua sehemu ndogo kwenye maeneo ya tumboni na
kuingiza mpira maalum ambao una kamera kwa mbele na huenda kuondoa uvimbe ulio
kwenye mayai ya mwanamke. Upasuaji huu hauachi kovu la aina yoyote ile
linalotokana na upasuaji, hivyo tiba ya aina hii hupendwa sana na
wanawake.
Je kuna madhara ya uvimbe kwenye
mayai ya mwanamke wakati wa ujauzito?
Tatizo la uvimbe kwenye mayai ya
mwanamke wakati wa ujauzito pia hutokea. Mara nyingi wanawake wajawazito
wenye uvimbe kwenye mayai ya yao huwa na uvimbe ambao siyo saratani. Kawaida
uvimbe kwenye mayai ya mwanamke wakati wa ujauzito hauna madhara yoyote yale
kwa mwanamke mjamzito au kwa kiumbe kilicho ndani ya tumbo kama ukiwa bado
mdogo.
Madhara
ya uvimbe kwenye mayai wakati wa ujauzito
- Uvimbe kuwa mkubwa sana na hivyo kusababisha maumivu makali kwa mjamzito, kama uvimbe huu utapasuka au kujinyonga wenyewe (twist on itself), basi kuna uwezekano wa mimba kuharibika na hivyo kutoka (miscarriage) au kujifungua mtoto mapema zaidi (pre- term labor).
- Kupasuka kwa uvimbe huu hakuleti madhara ya maambukizi yoyote yale.
- Dawa za kupunguza maumivu hutumiwa kwa wanawake wajawazito ambao hupata maumivu makali kutokana na kupasuka kwa uvimbe huu.
- Matumizi ya dawa za usingizi wakati wa kujifungua kwa mwanamke mjamzito mwenye uvimbe kwenye mayai yake bado ni salama
- Uvimbe huu ukiwa mkubwa na kujinyonga wenyewe au kukandamiza mfuko wa kizazi na hivyo kukandamiza kiumbe kilichomo ndani yake. Mwanamke mjamzito atahitaji upasuaji ili kuondoa uvimbe huu.Upasuaji hautamuathiri mama wala kiumbe kilicho ndani ya tumbo.Lakini kama unavyojua, wakati wa upasuaji kunaweza kutokea madhara yoyote yale, hivyo mwanamke mjazito wenye uvimbe kwenye mayai hushauriwa kuepuka upasuaji kama anaweza.
- Kama uvimbe huu utahitaji kufanyiwa upasuaji ili uondolewe, muda mzuri wa kufanyiwa upasuaji kwa mwanmke mjazito ni kuanzia wiki ya 13-28 ya ujauzito wake
- Uvimbe mdogo huweza kuondolewa kwa njia ya upasuaji ya Laparascopic surgery kama nilivyoeleza hapo juu, kwa uvimbe mkubwa, utahitaji kuondolewa kwa kufanyiwa upasuaji kwenye maeneo ya tumboni.
- Kutokana na uvimbe mkubwa kwenye mayai ya mwanamke kuwa na madhara mengi, mwanamke mjazito atahitaji uangalizi wa karibu kutoka kwa daktari.
- Kama mwanamke mjazito mwenye uvimbe kwenye mayai yake atatimiza miezi tisa ya ujauzito wake bila matatizo yoyote, anashauriwa ajifungue kwa njia ya upasuaji ili wakati wa upasuaji uvimbe ule nao pia uondolewe ili kumuepusha kufanyiwa upasuaji tena.
SULUHISHO
1.
Suluhisho
Linalopendwa.
Wanawake wengi baada ya kujifahamu kuwa homoni zao haziko sawa huenda
mahospitalini ambako hupewa madawa (bioidentical or synthetic hormones) na
wengine hufanyiwa hormone replacement therapy.
Tiba hii huandaliwa kwa ajili ya kuzifanya homoni zifanye kazi zake kama kawaida. Lakini hupelekea madhara yaliyotajwa hapo awali (juu).
2.
Suluhisho
La kudumu.
Mvurugiko wa homoni unasababishwa mara nyingi na upungufu wa lishe, msongo
wa
mawazo, na uwepo
wa
sumu mwilini na hivi vyote ni vitu unavyoweza
kurekebisha.
Kwa wanawake wenye changamoto
ya
mvuzugiko wa hormone mwilini,
tume
waandalia program ya lishe kamili na virutubisho muhimu. Program
hii
ni ya vyakula; sio
dawa wala miti shamba. Inasaidia kuweka sawa homone
za mwanamke, kuboresha mfumo
mzima wa uzazi,
kuleta heshima ya ndoa maana uke utarudi katika hali yake ya asili (mnato na ute ute ukeni wenye kuleta msisimko
wakati wa tendo
la
ndoa, na kupunguza kasi ya uzee). Sumu zikizidi mwilini mwanamke huzeeka kabla ya wakati na kupatwa na changamoto mbalimbali za kiafya ikiwemo:
vimbe zinazo
jipachika kwenye uzazi wa mwanamke, vidonda vya tumbo,
n.k.
Kwa yeyote anayehitaji hii program ya kuboresha na kuimarisha Afya yake
awasiliane na kampuni kwa namba zifuatazo.
+255 768 603 979.
TUMAINI NA SULUHISHO LA KUDUMU LIPO AMBALO NI:
BAADA YA CHANGAMOTO KUIKUMBA JAMII
JOPO LA WATAALAMU/MADAKTARI WALIOBOBEA KATIKA AFYA YA MWANADAMU WALIFANYA
TAFITI YA NAMNA YA KUONDOA CHANGAMOTO HII BILA KUTUMIA DAWA AU VIAMBATA VYENYE
SUMU BALI KUTUMIA VIRUTUBISHO.
Virutubisho
hivyo vimekuwa vikitumiwa na watu wengi kwa zaidi ya mataifa 170 duniani na
tunashuhuda nyingi za watu waliopata kuboreshwa kwa afya zao baada ya kutumia
virutubisho hivyo.
Kwa
Ushauri au Kupata Huduma zetu Kama Uko Dar Es Salaam,Dodoma,Arusha,Mwanza Na Mbeya,Rukwa,Katavi,Singina,Ruvuma,Njombe,Simiyu,Mara...na Popote Ulipo(Tanzania
Na Zaidi Ya Nchi 160 Duniani).
Free
delivery ndani ya Dar, kama upo mkoani utatumiwa pia ndani na nje ya tanzania .
Kwa
maelezo zaidi jinsi unavyoweza kupata bidhaa zinazo ondoa tatizo hilI wasiliana
nasi kupitia namba hii +255 768 603 979.
Ni
virutubisho asili ambavyo vimeshawasaidia watu wengi saana hapa nchini na
Duniani kwa Ujumla. Karibu Upate huduma zetu kwa ushauri pia wasiliana nasi
PIGA /TUMA NENO :"Health and wellness is Your Priority".kisha #SULUHISHO LA UVIMBE KWENYE MAYAI YA
MWANAMKE.
kwa
mawasiliano: +255 768 603 979..“
maamuzi yako ya sasa ni matokeo ya baadaye”
Kwa
kuelewa Zaidi,pitia hapa:
https://web.facebook.com/Yourhealthyourprioritylifestyles/…
https://web.facebook.com/MaishaNiAfyaLindaAfyaYako/
No comments:
Post a Comment
warmly welcome
contact us via +255 768 603 979.