Health And Wellness Is Your Priority & Personal Development Mentorship Programs.

“Your health is your responsibility, love your health as you love your stuff”. -@Paul Biswalo.

We are looking forward to connect with you.

Our phone number is +255 768 603 979,for only calls/text &
+255 ,for WhatsApp only.
Email-address : biswalopaul@gmail.com.

It's me your lovely friend,
Yours in faithfulness,

-@Paul Biswalo, C.E.O & FOUNDER.
Mentor || Motivational Speaker || Trainer || Event Host || Entrepreneur || Healthy & Life coach || Presenter & Inspirational Public Speaker.
*let's meet all at the Top because is no longer crowded*

SULUHISHO LA KUDUMU LA UGONJWA WA KASWENDE.

Kaswende ni nini?
Kaswende ni ugonjwa unaoambukiza haraka sana, mara nyingi kupitia ngono. Ugonjwa huu huenezwa kwa kugusa moja kwa moja mchubuko wa kaswende (syphilitic sore) uliopo kwenye ngozi, au kwenye ngozi laini zenye majimaji za ukeni, kwenye mkundu, na midomo. Kwa hiyo njia kuu ni kupitia ngono ya kawaida, ya kutumia midomo na ile ya kinyume na maumbile. Mara chache ugonjwa huu huweza kuambukiza kwa kubusiana au kugusana miili. Pamoja na kuwa ugonjwa huambukiza kupitia michubuko, mara nyingi michubuko hatarishi haitambulikani. Mtu aliyeambukizwa huwa hajielewi na hivyo kumwambukiza mpenzi wake.
Kaswende haiambukizi kwa kuchangia vyoo, vitasa vya milango, mabwawa ya kuogelea, kuchangia nguo au vyombo vya chakula.




Ugonjwa wa kaswende ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na bakteria aina ya Treponema pallidum.  Ugonjwa wa huu ni kati ya magonjwa ya zinaa yanayoongoza kwa kusababisha madhara mengi.

Maambukizi ya kaswende wakati wa ujauzito huleta madhara mengi sana kama kujifungua kiumbe ambacho kimeshakufa, mtoto kuathirika na ugonjwa huu wakati wa kuzaliwa, mtoto kupata matatizo wakati wa   ukuaji wake, degedege na kuongezeka kwa vifo vya watoto wachanga nchini. 
Ugonjwa wa kaswende huathiri zaidi ya mimba millioni moja duniani kote kila mwaka na huchangia theluthi mbili ya vifo vya watoto wale wanaozaliwa tayari wameshakufa katika nchi za maeneo ya jangwa la sahara. Asilimia 30 ya mimba zinazoathiriwa na kaswende huishia watoto kufariki wakati wa kuzaliwa. Asilimia nyengine 30 ya mimba zinazoathiriwa na kaswende husababisha watoto kuzaliwa na ugonjwa huu wa kaswende, kupata matatizo ya ukuaji wao, degedege na kuongeza vifo vya watoto kwa asilimia 50.



Taasisi ya  kudhibiti Ugonjwa wa Ukimwi Tanzania (Tanzania National AIDS Control Programme) au NACP imesema maambukizi yote ya kaswende wakati wa ujauzito Tanzania bara kati ya mwaka 2003 hadi 2004 ni asilimia 6.7, kutoka asilimia 0.4 kwa mkoa wa Kilimanjaro hadi asilimia 32 kwa mkoa wa Tabora katika ripoti yake ya utafiti uliofanywa chini ya Wizara ya afya na ustawi wa jamii. Maambukizi yalionekana yako juu zaidi kwa wanawake walio na umri wa miaka 35 na zaidi (7%) na kiwango cha maambukizi kuwa chini zaidi kwa wanawake walio na umri kati ya miaka 15 – 24 (6.5%).
Ugonjwa wa ukimwi na kaswende mara nyingi huambatana pamoja. Ugonjwa wa kaswende huongeza uwezekano wa mtu kupata ugonjwa wa ukimwi.

Visababishi vya ugonjwa wa kaswende
Kama tulivyosema awali, kaswende husababishwa na bakteria aina ya Treponema pallidum. Njia za maambukizi za ugonjwa huu ni kama zifuatavyo;
  • Kupitia kujamiana bila kutumia kinga na mtu aliyeambukizwa kaswende
  • Kujamiana kupitia njia ya haja kubwa (anal sex)
  • Kujamiana kupitia njia ya mdomoni (oral sex)
  • Mama aliyepata ugonjwa wa kaswende wakati wa ujauzito anaweza kumuambukiza mtoto wake wakati wa ujauzito.
  • Kuambukizwa kupitia michibuko au mipasuko kwenye ngozi wakati wa kujamiana au wakati mwengine wowote pale mtu anapogusana na mtu mwenye kaswende ikiwa wote wawili wana mipasuko kwenye sehemu mbalimbali za ngozi zao. Sio rahisi mtu kutambua kama ana michibuko au la kwenye ngozi kwani mengine inakuwa midogo sana isipokuwa ile ambayo inaweza kuonekana kwa macho.

  • Dalili na Viashiria vya ugonjwa wa kaswende
    Dalili na viashiria vya ugonjwa wa kaswende hutegemea na aina ya ugonjwa wa kaswende wenyewe. Kuna aina tano za ugonjwa wa kaswende ambazo ni;
    • Ugonjwa wa kaswende wa awali (Primary syphilis)
    • Ugonjwa wa kaswende wa pili (Secondary syphillis)
    • Kaswende iliyojificha (Latent syphilis)
    • Kaswende ya baadae (Tertiary syphilis)
    • Kaswende ya kurithi (Congenital syphilis)
      
    Kaswende ya awali (primary syphilis)
    Dalili ya kwanza ya aina hii ya kaswende ni kutokea kwa kidonda kidogo cha mviringo (chancre kama kinavyojulikana kitaalamu) katika sehemu ambayo bakteria wameingilia na hutokea kati ya siku 10 hadi miezi mitatu (kwa kawaida kuanzia wiki 2 hadi 6) baada ya mtu kupata maambukizi ya kaswende. Kidonda hiki kinaweza kutokea kwenye sehemu ya haja kubwa, shingo ya kizazi kwa wanawake (cervix), mdomoni (lips), uume (penis), ulimi, vulva, tupu ya mwanamke (vagina) na sehemu nyengine 
    mwilini.

     

    Tezi (lymph nodes) ambazo zipo karibu na sehemu iliyotokea kidonda hiki kawaida huwa zinavimba baada ya siku 7 hadi 10. Kidonda hiki hakiambatani na maumivu na kwa kuwa kinaweza kutokea katika sehemu zilizojificha kama kwenye shingo ya kizazi, sio rahisi mtu kutambua kama na aina hii ya kaswende. Kidonda hiki kinaweza kuwepo kwa muda wa wiki 3 hadi 6 kama mtu hatapata tiba na kinatoweka chenyewe bila tiba au baada ya kupata tiba.
    Robo tatu ya wale ambao hawapati tiba huishia kuingia kwenye kundi la kaswende ya aina ya pili (Secondary syphilis).

     

    Kaswende aina ya pili (Secondary syphilis)
    Aina hii hutokea wiki 4 hadi 10 baada ya mtu kupata kaswende ya awali. Dalili za aina hii ya kaswende ni;
    • Vipele ambavyo haviwashi katika viganja vya mikono au nyayo za miguu. Vipele hivi pia vinaweza kutokea mwili mzima au sehemu mbalimbali za mwili.
    • Uchovu
    • Kuumwa  kichwa
    • Homa (fever)
    • Kunyofoka  nywele
    • Vidonda vya koo (sore throat)
    • Kuvimba kwa matezi mwili mzima
    • Maumivu ya mifupa (joint pain)
    • Kupungua uzito
    Kaswende ya aina hii inakuwepo kwa wiki kadhaa na hupotea hata bila kupata tiba kwa mtu aliyeathirika. Pia inaweza kujirudia rudia katika kipindi cha mwaka mmoja hadi miwili na mtu huingia kwenye kundi la aina ya tatu ya ugonjwa wa kaswende (latent syphilis) baada ya miaka miwili.

     

    Kaswende iliyojificha (Latent syphilis)
    Hii inajulikana kama kaswende ambayo inaweza kutibika tu kwa kutumia vipimo vya maabara (serological test). Imegawanyika katika makundi mawili:
    i. Early latent syphilis (kaswende iliyojificha ya awali) – Hii ni ile ambayo hutokea ndani ya kipindi cha mwaka mmoja baada ya muathirika kuugua kaswende aina ya pili (secondary syphilis). Aina hii huwa na dalili zinazojirudia kama za kaswende ya pili (secondary syphilis)
    ii.  Late latent syphilis (kaswende iliyojificha ya kuchelewa) – Hii hutokea baada ya mwaka mmoja wa kuugua kaswende ya aina ya pili (secondary syphilis). Wakati wa kuugua aina hii, muathirika anakuwa hana dalili wala viashiria vyovyote vile na uwezo wake wa kuambukiza mtu mwengine unakuwa chini au hawezi kabisa kumuambukiza kaswende mtu mwengine.

     

    Kaswende ya baadae (Tertiary syphilis)   
    Asilimia 30 ya wagonjwa wa kaswende ambao hawakupata tiba hapo awali huingia kwenye kundi hili na hutokea miaka 15 – 30 baada ya maambukizi ya kaswende hapo awali. Aina hii inaweza kuathiri viungo kama macho, ubongo, mishipa ya fahamu (Neurosyphilis), jointi au viunganishi vya mifupa, uti wa mgongo, moyo, mishipa ya damu na hivyo kusababisha madhara makubwa kama;

    • Upofu
    • Magonjwa ya moyo – Aortic dissection type B, syphilitic aortitis
    • Magonjwa ya akili
    • Magonjwa ya mishipa ya fahamu
    • Mtu kuwa kiziwi
    • Kupungukiwa na kumbukumbu (Memory loss)
    • Kifo
    Pia aina hii ya kaswende inaweza kuathiri mfumo wa chakula (abdominal organs), mfumo wa kupumua (respiratory system) na mfumo wa uzazi (reproductive system).

    Kaswende ya kurithi (Congenital  syphilis)
    Aina hii hutokea wakati wa ujauzito au baada ya mtoto kuzaliwa. Robo mbili ya wototo wanaozaliwa hawaonyeshi dalili zozote. Nusu ya watoto wenye maambukizi ya kaswende hufariki muda mfupi kabla ya kuzaliwa au baada ya kuzaliwa. Dalili za aina hii ya kaswende kwa mtoto mchanga zinaweza kutokea baada ya kuzaliwa au wiki 2 hadi miezi 3 baada ya kuzaliwa;
    • Kutoongezeka uzito au kushindwa kukua
    • Homa
    • Kukasirika haraka (irritability)
    • Kutochongoka kwa pua, pua inakuwa bapa (no bridge to nose or saddle nose)
    • Vipele kwenye viganja vya mikono na kwenye  nyayo
    • Vipele vya rangi ya madini ya shaba kwenye uso, viganja vya mikono na nyayo
    • Vipele kwenye mdomo, sehemu za siri na sehemu ya haja kubwa
    • Kutokwa na majimaji puani
    • Kuongezeka ukubwa wa ini na bandama (hepatosplenomegally)
    • Ngozi kuwa ya njano (jaundice)
    • Upungufu wa damu mwilini (anemia)

    Dalili kwa mtoto mkubwa
    • Kuathirika meno (Hutchinson teeth)
    • Maumivu ya mifupa
    • Upofu
    • Kupungua uwezo wa kusikia au mtoto kuwa kiziwi
    • Ukungu kwenye mboni za macho (Clouding of cornea)
    • Vidonda rangi ya kijivu kwenye sehemu ya haja kubwa na kwenye tupu ya mwanamke (vagina)
    • Ngozi kuwa na mabaka meusi kwenye mdomo, sehemu za siri na sehemu za haja kubwa
    • Maumivu kwenye mikono na miguu
    • Kuvimba jointi za mifupa

    Ugunduzi wa ugonjwa wa kaswende
    Ugunduzi wa ugonjwa wa kaswende huusisha utambuzi wa dalili na viashiria vya ugonjwa huu (hii hufanywa na daktari) kupitia historia ya mgonjwa, vipimo vya damu na vipimo vya kugundua bakteria aina ya Treponema pallidum.

    Utambuzi wa dalili na viashiria vya ugonjwa wa kaswende
    • Hufanywa na daktari
    • Huusisha historia ya mgonjwa

    Vipimo vya damu
    Vipimo hivi vinahusisha utambuzi wa chechembe za antibodies dhidhi ya bakteria Treponema pallidum. Majibu yanaweza kuwa false positive (Wale ambao vipimo vimeonyesha wana kaswende lakini hawana ugonjwa huu,hii hutokea kwa wale ambao waliugua kaswende awali na hali hii inaweza kuwepo hadi miezi mitatu baada ya kupona ugonjwa huu au wale wenye ugonjwa wa kifua kikuu, malaria, wajawazito, measles, endocarditis, connective tissue disease nk.) au false negative (Wale ambao wameathirika na kaswende lakini vipimo vinaonyesha hawana kaswende). Mara nyingi ni vigumu sana kuthibitisha uwepo wa ugonjwa huu, hivyo vipimo hurudiwa ili kupata uthibitisho.
    • RPR (Rapid plasma reagin) test
    • VDRL (Veneral Disease Research Laboratory)
    • The microhemagglutination assay [MHA-TP] Hufanywa kuthibitisha ugonjwa wa kaswende
    • Fluorescent-treponemal-antibody absorption [FTA-ABS, enzyme-linked immunosorbent assay ELISA])  Hufanywa kuthibitisha ugonjwa wa kaswende
    • PCR (Polymerase Chain Reaction) – Kipimo cha kuangalia vina saba (DNA) vya Treponema pallidum.
    • Complete Blood Count - Kipimo cha kuangalia wingi wa damu na aina tofauti za chembechembe za damu

    Vipimo vya kugundua bakteria
    Hufanywa kwa kutumia hadubini ( Dark field microscopy).

    Vipimo kwa wale wenye madhara ya kaswende
    • Picha ya X-ray ya kifua, uti wa mgongo
    • Vipimo vya moyo – ECG, transesophageal echocardiogram,aortic angiography, doppler ultrasonography, chest MRI, cardiac CT scan (contrast), CT angiography.
    • CT scan ya kichwa, mfumo wa chakula (abdominal CT)
    • MRI ya kichwa, uti wa mgongo, brainstem
    • Bone scan (Vipimo vya mifupa)
    • Vipimo vya macho
    • Vipimo vya masikio
    • Lumbar puncture – Kipimo cha kuangalia bakteria kwenye maji ya uti wa mgongo
    • Cerebral angiogram – Kipimo cha kuangalia mishipa ya damu kwenye ubongo
    • Nerve conduction tests

    Tiba ya ugonjwa wa kaswende
    Kwa zamani iliaminika kuwa Tiba ya ugonjwa wa kaswende inahusisha matumizi ya dawa za antibiotic za kundi la penicillin. Dawa nyengine ni aina ya polyketides antibiotics (doxycyline nk.)  lakini hizi hazitumiki kwa wajawazito. Kwa wale ambao wanapata madhara baada ya kutumia penicillin ni bora kumjulisha daktari mapema. Tiba kwa wale wenye kaswende iliyoathiri mishipa ya fahamu ni penicillin inayotolewa kupitia kwenye mishipa ya damu na wanahitaji kulazwa hospitali kwa matibabu zaidi. Wale ambao wameathiriwa na kaswende kwenye viungo vya mwili, madhara hayo sio rahisi kurekebishika na mengine hayarekebishiki.

    ANGALIZO.
    Kwa sasa Ugonjwa Wa Kaswende Wadaiwa Kuwa Sugu Kwa Dawa za hospitalini,
    Tangu Tarehe July 7, 2017 ya mwaka jana inasemekana bakiteria hawa kuwa sugu kwa matumizi ya dawa za hospitalini,hivyo inatakiwa kutumia VIRUTUBISHO ambavyo ndio vinaaminika kuwa na uwezo wa kukabiliana na bakiteria hawa ambao wamekuwa sugu kwa dawa za hospitalini kama penicillin, polyketides antibiotics.virutubisho hivi,ni Zaidi ya dawa maana ni chakula ambavyo havina sumu za kikemikali kama zilivyo dawa za hospitali,na zimeleta matokeo chanya na makubwa sana katika kupambana na tatizo hili.


    Dalili za kaswende za sasa Tangu Tarehe July 7, 2017 ya mwaka jana,hii ni kutokana na tafiti za Shirika la Afya Duniani (WHO).

    Kaswende sasa inazidi kuwa ugonjwa sugu usiotibika hata kwa viuavijisumu (antibiotics), Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema.
    “Bacteria wasababishao ugonjwa wa kaswende ni werevu sana. Kila mara tunapotumia viuavijisumu kutibu maambukizi, ndivyo
    bacteria hao wanavyojibadili kukabiliana na viuavijisumu hivyo,” anasema Teodora Wi, mwakilishi wa WHO amesema.

    Ugonjwa Wa Kaswende Wadaiwa Kuwa Sugu Kwa Dawa - Tanzania -
    Ametahadharisha kuwa watu wanapaswa kuwa makini kwakuwa tatizo hilo limezidi kuwa sugu kadiri siku zinavyozidi na vimelea (backteria) waliopo hawawezi kuuliwa na dawa bora zilizopo sasa.

    Wadudu watatu (vimelea) ambavyo haviwezi kuuliwa na dawa bora zipatikanazo sasa waligundulika nchini Japan, Ufaransa
    na Uhispania, kwa mujibu wa WHO.
    “Kila mwaka watu zaidi ya Milioni 78 wanahisiwa kuambukizwa ugonjwa wa Kaswende,” WHO inasema.

    Tiba ya upasuaji
    Tiba ya upasuaji kwa wale wenye madhara ya ugonjwa wa kaswende kama kwenye moyo na nk.
    Wagonjwa wa syphilitic aortitis wanaweza kutibiwa kwa angiography/angioplasty lakini kama wana magonjwa mengine ya moyo kama coronary heart disease basi tiba hii haifanyiki.

    Madhara ya ugonjwa wa kaswende
    • Magonjwa ya moyo                                        
    • Magonjwa ya akili
    • Mtu kuwa kiziwi
    • Upofu
    • Magonjwa ya mishipa ya fahamu
    • Kupungukiwa kumbukumbu (memory loss)
    • Upungufu wa damu mwilini
    • Mimba kutoka wakati wa ujauzito
    • Kuzaa mtoto ambae ameshafariki
    • Madhara kwenye mifupa
    • Vifo vya watoto

    Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa kaswende
    • Kufanya ngono salama kwa kutumia kondomu, njia sahihi ni kuepuka kabisa ngono
    • Wale walioathirika kuacha kufanya ngono na wenza wao hata kama wameanza tiba mpaka vidonda vipone
    • Kwa wajawazito, kuhudhuria kliniki mapema ili kama ukigundulika kuwa na kaswende hivyo kupata tiba haraka.
    • Epuka kugusana na majimaji yoyote yanayotoka kwa mtu aliyeathirika kwa ugonjwa huu.

    TUMAINI NA SULUHISHO LA KUDUMU LIPO AMBALO NI:
    BAADA YA CHANGAMOTO KUIKUMBA JAMII JOPO LA WATAALAMU/MADAKTARI WALIOBOBEA KATIKA AFYA YA MWANADAMU WALIFANYA TAFITI YA NAMNA YA KUONDOA CHANGAMOTO HII BILA KUTUMIA DAWA AU VIAMBATA VYENYE SUMU BALI KUTUMIA VIRUTUBISHO.

    Virutubisho hivyo vimekuwa vikitumiwa na watu wengi kwa zaidi ya mataifa 170 duniani na tunashuhuda nyingi za watu waliopata kuboreshwa kwa afya zao baada ya kutumia virutubisho hivyo.

    Kwa Ushauri au Kupata Huduma zetu Kama Uko Dar Es Salaam,Dodoma,Arusha,Mwanza Na Mbeya,Rukwa,Katavi,Singina,Ruvuma,Njombe,Simiyu,Mara...na Popote Ulipo(Tanzania Na Zaidi Ya Nchi 160 Duniani).
    Free delivery ndani ya Dar, kama upo mkoani utatumiwa pia ndani na nje ya tanzania .

    Kwa maelezo zaidi jinsi unavyoweza kupata bidhaa zinazo ondoa tatizo hili
     wasiliana nasi kupitia namba hii +255 768 603 979.

    Ni virutubisho asili ambavyo vimeshawasaidia watu wengi saana hapa nchini na Duniani kwa Ujumla. Karibu Upate huduma zetu kwa ushauri pia wasiliana nasi PIGA /TUMA NENO :"Health and wellness is Your Priority".kisha #SULUHISHO LA KUDUMU LA UGONJWA WA KASWENDE.

    kwa mawasiliano: +255 768 603 979..“ maamuzi yako ya sasa ni matokeo ya baadaye”

    Kwa kuelewa Zaidi,pitia hapa:
    https://web.facebook.com/Yourhealthyourprioritylifestyles/…
    https://web.facebook.com/MaishaNiAfyaLindaAfyaYako/
    https://paulbiswalo.blogspot.com/
    https://www.pinterest.com/biswalopaul/
    SHARE NA UNAOWAPENDA ILI WAFAIDI ELIMU HII YA BURE.

    KWA KUENDELEA KUPATA UP-DATE JUU YA AFYA LIKE PAGE HII NA KUSHARE ELIMU HII YA BURE KWA WENGINE ILI NAO WAPATE ELIMU HII KWA FAIDA YA AFYA YAO.

Share:

No comments:

Post a Comment

warmly welcome

contact us via +255 768 603 979.

Popular Posts

Blog Archive

for any assistance.

“Your health is your responsibility, love your health as you love your stuff”. -@Paul Biswalo.

We are looking forward to connect with you.

Our phone number is +255 768 603 979,for only calls/text &
+255 ,for WhatsApp only.
Email-address : biswalopaul@gmail.com.

It's me your lovely friend,
Yours in faithfulness,

-@Paul Biswalo, C.E.O & FOUNDER.
Mentor || Motivational Speaker || Trainer || Event Host || Entrepreneur || Healthy & Life coach || Presenter & Inspirational Public Speaker.
*let's meet all at the Top because is no longer crowded*

Featured post

UNAFAHAMU UMUHIMU NA FAIDA YA KUBORESHA KINGA YA MWILI??????

AFYA YAKO NI JUKUMU LAKO. UNAFAHAMU UMUHIMU NA FAIDA YA KUBORESHA KINGA YA MWILI?????? jiulize swali hili na utafakali vizuri ilik...

Followers

Contact Form

Name

Email *

Message *

Labels

Total Pageviews

Theme Support