KAMA WEWE NI MPENZI WA KUSOMA VITABU TAFADHALI JIFUNZE KITU HAPA
UNAHITAJI KITABU ZAIDI YA UNAVYOWEZA KUDHANI.
�〰�〰�〰�
©Habel Samida:
Mwandishi na Mhamasishaji.
Umeshafanikiwa kuandika kitabu? Kama umefanikiwa HONGERA SANA. Kama bado, umeshawahi kuwaza kuandika?
Ukweli ni kwamba, unahitaji sana kuandika kitabu. Unaweza kujiuliza "kwanini niandike kitabu? Naanzaje?" Majibu yote yako hapa.
Nilieleza hapo awali kwamba, unahitaji sana kuandika kitabu zaidi ya vile unavyoweza kufikiria. Zifuatazo ni baadhi ya sababu; kwanini uandike kitabu.
1. Una kitu ambacho wengine wanatamani kukifahamu.
2. Kitabu kitaendelea "kuishi" hata wewe usipokuwepo juu ya uso wa dunia. (Kitaacha alama zako)
3. Utaaminika na kuchukuliwa kama mtu uliyebobea au naweza kusema "professional".
Nimejifunza kwamba, unapokuwa umeandika kitabu, mtazamo wa watu juu yako hubadilika. Thamani yako huongezeka, kwakuwa umethubutu kufanya jambo ambalo asilimia ndogo sana ya watu duniani huwa na ujasiri wa kulifanya.
Licha ya hivyo, utaaminika zaidi, ukizingatia kuwa; watu wanaamini sana katika kile wanachokisoma kuliko kusikia! Kwa mfano; kama unasimulia ajali iliyotokea mahali Fulani, ambapo uliishuhudia halafu akaja mtu mwingine akaanza kukubishia kwamba haikuwa hivyo! Akatoa gazeti ambalo limeripoti habari hiyo.
Kiuhalisia mtu huyo atakuwa sahihi kwakuwa ana ushahidi. Hata kama mwandishi aliyeripoti habari hiyo hakuwepo kushuhudia tukio.
Ni kwa sababu, watu wanaamini sana katika kile wanachokisoma.
4. Kitabu kitafungua milango mingi ambayo hukutegemea.
Hii ni mbinu aliyonifundisha mwalimu wangu Rene katika tasnia ya uhamasishaji. Alianza kuandika kitabu akiwa ameajiriwa kama mfagizi katika hoteli. Baada ya kuandika kitabu chake, kilifungua milango mingi sana. Aliitwa kwenye vituo vya redio na televisheni mbali mbali na kupata mialiko kuongea katika mikutano mbalimbali.
Hapo maisha yake hayakubaki vile yalivyokua.
Nimeshuhudia kwangu pia, nilipofanikiwa kuandika kitabu cha JAHILI, kilinifanya nikutane na watu ambao sikutarajia.
No comments:
Post a Comment
warmly welcome
contact us via +255 768 603 979.