Health And Wellness Is Your Priority & Personal Development Mentorship Programs.

“Your health is your responsibility, love your health as you love your stuff”. -@Paul Biswalo.

We are looking forward to connect with you.

Our phone number is +255 768 603 979,for only calls/text &
+255 ,for WhatsApp only.
Email-address : biswalopaul@gmail.com.

It's me your lovely friend,
Yours in faithfulness,

-@Paul Biswalo, C.E.O & FOUNDER.
Mentor || Motivational Speaker || Trainer || Event Host || Entrepreneur || Healthy & Life coach || Presenter & Inspirational Public Speaker.
*let's meet all at the Top because is no longer crowded*
TRUMP: HIZI NDO SIRI ZA KUTOSHINDWA KWENYE BIASHARA!
Unawapomzungumzia wanasiasa wenye mkwanja mrefu duniani, huwezi kuliacha jina la Donald John Trump ambaye wiki iliyopita alishinda kiti cha Urais wa Marekani kupitia chama chake cha Republican kwa kumwangusha mwenzake wa Chama cha Democrat, Hillary Clinton. Kwa ushindi huo, Januari 20, mwakani, ataapishwa kuwa rais wa nchi hiyo.
Ukiachilia mbali masuala ya kisiasa akiwa ameitikisa dunia, Trump ana mkwanja wa maana. Ana vitega uchumi kibao vikiongozwa na hoteli nyingi kama Turnberry iliyopo Ayshire nchini Scotland, Trump International zilizopo New York, Las Vegas, Chicago zote zikiwa nchini Marekani na nyingine nyingi.
Trump ni tajiri, bilionea ambaye leo hii naye anatamani kukuona ukiondoka katika umaskini na kuwa bilionea kama alivyo yeye.
Unajua kwa nini Trump alifanikiwa? Unajua alipitia njia zipi hadi akafanikiwa? Msome hapa akikupa siri za kufanikiwa;

USIFANYE VITU, KISA FEDHA
Katika masomo yake ya utajiri, Trump anafundisha: “Nimekuwa kwenye changamoto nyingi. Mara nyingi watu wamekuwa wakifanya mambo mengi kwa sababu wanahitaji fedha. Ndugu yangu, sikuwahi kufanya biashara ili nipate fedha, nimekuwa nikifanya biashara kwa sababu napenda biashara.
Unapofanya kitu kwa ajili ya fedha, ukizikosa itakuwaje? Si utaachana nayo? Sasa ili usiachane nayo, usifanye kwa ajili ya fedha, fanya kwa sababu unapenda kufanya.

USIKATE TAMAA
Nilipokuwa ninasoma chuoni, nilikuwa na marafiki waliokuwa na akili nyingi. Pia niliwahi kuwa na marafiki ambao hawakuwa na akili nyingi. Leo hii, wale waliokuwa na akili nyingi, hawana uwezo mkubwa kifedha, lakini wale ambao hawakuwa na akili nyingi, leo hii ni wafanyabiashara wakubwa.
Kilichowafanya wenye akili nyingi kutokuwa na uwezo wa kifedha ni kwa sababu walikata tamaa. Walipambana, ndiyo, ila walifika sehemu hawakuona kama wangefanikiwa hivyo kuachana na biashara, ila wale wengine walipambana, hawakurudi nyuma, walipoanguka, walinyanyuka na kuendelea hadi wakafanikiwa. Hicho ndicho unachotakiwa kufanya. Kamwe hutakiwi kukata tamaa.

ANDIKA KILA KITU
Kwenye biashara ni muhimu sana kuandika kila kitu. Kama unataka kufanya biashara au wewe ni mfanyabiashara, unatakiwa kuandika kila kitu. Leo zimeingiza kiasi gani? Andika, leo nimepoteza kiasi gani? Andika. Ukifanya hivyo utajua jinsi biashara inavyokwenda, utajua kama inashuka au inapanda kwa sababu utakuwa na hesabu zote. Mimi sikuwahi kufanya biashara bila kuandika, nimekuwa nikiandika hata kama nitatumia dola moja kwa ajili ya chakula.

KUWA NA WAFANYAKAZI WENYE KIU YA KUENDELEA
Wakati mwingine wafanyakazi wamekuwa wakiturudisha nyuma, wamekuwa hawajitumi kama inavyotakiwa. Ndugu yangu, unapokuwa na wafanyakazi wavivu, huwezi kusonga mbele, unapokuwa na watu wasiokuwa na mawazo mapya, huwezi kusonga mbele. Ni lazima uwe na timu yenye nguvu ambayo itakutoa hapo ulipo na kukupeleka sehemu nyingine. Kama ikitokea mfanyakazi hafanyi kile unachotaka akifanye, achana naye kwani bila hivyo, hutapiga hatua.

FANYA KAZI KWA KUJITUMA
Hutakiwi kuwa mvivu, unatakiwa kufanya kazi kwa kujituma kila siku. Nimekuwa nikifanya hivyo miaka yote, sikuwahi kuwa mvivu. Kuna watu wanatamani kuwa na mafanikio lakini wamekuwa hawataki kujituma, wamekuwa hawataki kufanya kazi kwa bidii na mwisho wa siku wamejikuta wakianguka na kurudi nyuma. Ili ufanikiwe zaidi, hutakiwi kuwa mvivu, hutakiwi kuzorota, unatakiwa kuwa na nguvu ya kujituma kila siku iendayo kwa Mungu na utafanikiwa.

NI LAZIMA UYAFUATE MALENGO
Kwanza unatakiwa kujiwekea malengo yako na mwisho wa siku kuyafuata malengo hayo. Hutakiwi kuyumba na kuyaacha. Labda kuna watu watakuambia kwamba unapotea, hutakiwi kuwasikiliza kwa kuamini kwamba kuyafuata malengo hayo ndiyo njia mojawapo ya kufanikiwa. Ukianza kuyumbishwa na watu na kuyaacha malengo yako, kamwe huwezi kufanikiwa.

JIAMINI
Unatakiwa kujiamini kwa kila kitu unachokifanya. Nimewaona wengi wakifeli kwa sababu hawakutaka kujiamini. Wengi wamekuwa wakirudi walipokuwa kwa sababu hawakuwa wakijiamini. Mimi ninajiamini, sipendi kushindwa, sijawahi kushindwa na kamwe sitashindwa kwa sababu ninajiamini. Kama ukitaka kufanikiwa, huna budi kujiamini, ukifanikiwa katika hilo, utake usitake utafanikiwa tu katika biashara zako.”

UTAJIRI WAKE SASA
Trump sasa ni bonge la bilionea. Utajiri wake unakadiriwa kufikia dola bilioni 3.7 (zaidi ya shilingi trilioni 7). Amewekeza sehemu nyingi na amekuwa akitajirika kadiri siku zinavyozidi kwenda mbele.
Wewe ni mtu maalumu,
Wewe una NGUVU,UWEZOna THAMANI ndani yako. ONDOA hofu katika kukamilisha mafanikio yako.

follow through this link to get more inspirational words:https://paulbiswalo.blogspot.com/
Ni Mimi rafiki yako mpendwa,
Paul Biswalo,
Mwalimu, Mhamasishaji &mtia moyo wa wote na mzungumzaji .
*karibuni wote kwenye kilele cha mafanikio Maana hakijajaa*

#*karibuni wote kwenye kilele cha mafanikio Maana hakijajaa*#

Share:

No comments:

Post a Comment

warmly welcome

contact us via +255 768 603 979.

Popular Posts

Blog Archive

for any assistance.

“Your health is your responsibility, love your health as you love your stuff”. -@Paul Biswalo.

We are looking forward to connect with you.

Our phone number is +255 768 603 979,for only calls/text &
+255 ,for WhatsApp only.
Email-address : biswalopaul@gmail.com.

It's me your lovely friend,
Yours in faithfulness,

-@Paul Biswalo, C.E.O & FOUNDER.
Mentor || Motivational Speaker || Trainer || Event Host || Entrepreneur || Healthy & Life coach || Presenter & Inspirational Public Speaker.
*let's meet all at the Top because is no longer crowded*

Featured post

UNAFAHAMU UMUHIMU NA FAIDA YA KUBORESHA KINGA YA MWILI??????

AFYA YAKO NI JUKUMU LAKO. UNAFAHAMU UMUHIMU NA FAIDA YA KUBORESHA KINGA YA MWILI?????? jiulize swali hili na utafakali vizuri ilik...

Followers

Contact Form

Name

Email *

Message *

Labels

Blog Archive

Total Pageviews

Theme Support