UFAHAMU UGONJWA WA HOMA YA INI
(MCHOCHOTA WA INI).
A. Ini ni nini ?
Ini ni miongoni mwa kiungo muhimu katika mwili wa binadamu, ya pili kwa
ukubwa katika viuongo vyote, ya kwanza ikiwa ni ngozi. Ini linapatikana kwenye
kivambi cha mbavu upande wa kulia, uzito wake ni kuanzia 1 kg – 1.5 Kg. Faida
kubwa ya ini inasaidia kutoa vimeng’enyo vya chakula na kuondoa baadhi ya sumu
mwilini. Ni mojawapo kati ya viungo vinavyohusika katika kutoa uchafu, uhifadhi
wa chakula katika mwili wa binadamu. Chakula kinapotaka kuingia mwilini katika
utumbo mwembamba huelekea kwanza katika ini.
B. Homa ya ini
Virusi vya homa ya Ini ni hatari zaidi ya virusi vya Ukimwi
Virusi vya homa ya ini (hepatitis) – kwa kiswahili mchochota wa ini; kazi yake
nikuharibu cell za ini. Baada ya kuharibu cell za ini ndo vinaenea kwenye damu.
Homa ya Ini ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoshambulia
ini.
Virusi hivi ni vya aina kuu tano A, B, C, D na E. Maambukizi yake niya kimya
kimya. Ili uweze kuona dalili inachukua muda mrefu. Dalili zikishatokea ini
linakuwa limeshaathirika zaidi.
Tafiti zinaonesha ugonjwa huu ni hatari zaidi ya ugonjwa wa UKIMWI kwasababu
virusi vyake vinauwezo wakuishi nje ya mwili wa binadamu kwa muda mrefu zaidi
ya siku saba, na ni rahisi sana kuambukizwa.
Kwa upande wa Tanzania watu wengi hawana ufahamu na ugonjwa huu. Takwimu
zilizochukuliwa katika baadhi ya makundi mbali mbali, zinaonesha kwamba
wagonjwa wa virusi vya ukimwi wako kwenye hatari ya kuambukizwa kwa urahisi
ugonjwa huu, na kuchochea kuathirika zaidi hata kufa mapema kwasababu kinga
ya miili yao iko chini. Wagonjwa wa ukimwi wakipata vitu vya kuboost kinga ya
mwili itasaidia kuongeza uwezo wa mwili kujilinda zaidi na magonjwa hatarishi
yanayoshambulia kinga ya mwili na hivyo kumsaidia kutoathirika zaidi na virusi
vya ukimwi.
II. VYANZO VYA HOMA YA INI
Kirusi cha homa ya Ini kinauwezo wa kukaa nje ya mwili wa binadamu vikiwa hai
hata zaidi ya miezi mitatu
Chanzo cha Homa ya Ini inayosababishwa na virus 1. wa aina ya A & E:
- Kula kinyesi kilichochanganyika na aina hii ya vimelea kwenye maji au
chakula
Vyanzo vya Homa ya Ini inayosababishwa na Virus wa aina ya B, C &
D:
Mchanganyiko wa damu ambao hutokana na:
· Ngono zembe
· Wakati wa kusafisha figo ya mtu mwenye homa ya Ini
· Kuchangia damu isiyo salama
· Wakati wakuwekewa damu
· Kupitia mama mwenye maambukizi kwenda kwa mtoto: Mama mwenye
maambukizi anauwezo mkubwa wa kumuambukiza mtoto akiwa tumboni, na
wakatibwa kujifungua.
Ushirikiano wa vitu vya kila siku
· Kushirikiana vitu vyenye ncha kali (sindano, nyembe, chanjo, hereni..etc)
· Mate: kunyonyana ndimi
· Kuchangia taulo na mtu mwenye ugonjwa huu
· Kuchangia miswaki
· Kwa njia ya jasho
· Kuchangia nguo na mwenye ugonjwa huo
III. DALILI ZA HOMA YA INI
Kwasababu tumeumbwa kwa aina tofauti ya makundi ya damu, asilimia kubwa ya
watu hawaoni dalili yoyote kutokana na makundi yao ya damu; hivyo ni rahisi
kuishi na virusi vya homa ya Ini na kuambukiza wengine kirahisi hata bila wewe
kujua. Endapo dalili zitajitokeza; ili uzione, itakuchukua takribani kati ya siku 30
– 180 baada ya kupata maambukizi ya virus vya ini. Dalili hizi hazina utofauti na
dalili za malaria, na chaajabu dalili hizi hazikai kwa muda, huwa zinakuja na
kupotea.
Dalili hizi siyo maranyingi zinawapata watu. Huu ni ugonjwa wa kimya kimya, na
unakuua bila kujua. Mtu anaweza kupata maambukizi ya virusi vya homa ya ini
lakini asipate dalili kwa wakati huo, na baadae zinaweza kuonekana hizo dalili
wakati homa ya ini imeshakuwa sugu.
- Homa kali sana, na muda mwingine inajirudia mara kwa mara
- Uchovu wa mara kwa mara
- Kuishiwa nguvu: kujihisi mwili dhaifu
- Kupungua uzito ghafla na mwili kudhoofika
- Mkojo mweusi
- Macho na ngozi kuwa vya njano
- Kichefuchefu
- Kutapika
- Maumivu makali ya tumbo upande wa Ini
- Kuharisha
IV. MADHARA YA HOMA YA INI
Katika hatua ya mwisho virusi vya homa ya ini husababisha mgonjwa kupata
saratani ya ini.
- Ini kupata vidonda, kusinyaa na kuwa dogo zaidi: Hii hupelekea ini
kushindwa kufanya kazi vizuri na mwishowe kupata saratani ya ini.
- Kutapika na kutoa kinyesi chenye damu: Ini likisinyaa linazuia mishipa
kupitisha damu. Mishipa inayopeleka damu kwenye ini italazimika kutoa damu
kupitia mishipa ilio kwenye koo la chakula. Mishipa ya koo ni laini sana hivyo
hushindwa kustahimili damu hiyo na kupasuka.
- Ini kuoza
- Ini kushindwa kufanya kazi yake
- Kifo
V. SULUHISHO LA HOMA YA INI
Kutokana na tafiti zilizopo mpaka sasa tiba ya homa ya ini haipo, isipokuwa kuna
dawa za hospital (kemikali) zinasaidia kupambana na virusi ili vipunguzwe makali
na sio kuongeza au kuboresha kinga ya mwili. Kutokana na kemikali zilizo kwenye
dawa ulizotumia, hupelekea kinga yako ya mwili kuzidi kudhoofika, na baadae
kupatwa na matatizo mengine ya kiafya.
Vyakula tunavyokula viko aina 3. Kuna vyakula tukivipata vinaongeza kinga ya
mwili, vingine vinabaki kuwa kama vyakula tu hatunufaiki chochote, vingine
vinakuwa sumu mwilini kwetu. Tunafaa kula vyakula vinaendana na makundi ya
damu yetu ili afya zetu zizidi kuwa imara zaidi.
Kutokana na mfumo wa maisha jinsi ulivyo na namna vyakula vinavyolimwa
hatupati mlo kamili, ndio mana tunalazimika kutumia virutumbisho ili mwili
uweze kupata vitu vyote vinavyohitajika. Mwili wenyewe unauwezo
wakutengeneza kinga endapo utapata virutubisho.
Faida ya Virutubisho hivi
Virutubisho hivi huwa na madini, vitamin, protini, amino acids na virutubisho vya
kambakamba ambavyo ni muhimu zaidi katika kuimarisha kinga ya mwili.
- Husaidia katika kuua bacteria na virusi nyemerezi ambao huathiri ini
(kitendo hiki kinasababisha ini kurudi katika ubora wake - normal)
- Husaidia katika kuboresha na kuimarisha kinga ya mwili (Utaisha maisha
marefu endapo kinga ya mwili itakuwa bora na imara). Afya haitadhoofika
- Husaidia katika kuondoa maumivu na uchovu wa mara kwa mara
- Husaidia katika kurudisha ubora wa seli za mwili, na kuboresha utendaji kazi
wa seli za mwili
- Husaidia katika kuongeza nguvu na kuboresha mmeng’enyo wa chakula
- Husaidia kupunguza kiwango cha mafuta ambayo hupelekea saratani
Kwa yeyote anayehitaji hivi virutubisho vya kuboresha na kuimarisha afya
yake ya Ini awasiliane na kampuni kwa namba zifuatazo:+255 768 603 979.kwa msaada zaidi.
No comments:
Post a Comment
warmly welcome
contact us via +255 768 603 979.