ZITAMBUE DALILI ZA SARATANI YA TITI
Kutambua jinsi titi lako linavyotakiwa kuwa katika hali ya kawaida, ni jambo muhimu sana kwa afya yako ya titi. Unapoitambua saratani ya titi mapema, unakuwa katika nafasi kubwa sana ya kuitibu.
Dalili ya kwanza ya saratani ni uvimbe. Uvimbe ambao hauna maumivu, ni mgumu, una mikunjo mikunjo, mara nyingi hiyo ni dalili ya saratani, lakini saratani za titi zinaweza kuwa laini, ororo, au mviringo. Uvimbe unaweza kuwa hata wenye maumivu pia.
Ni vizuri unapoona badiliko lolote kwenye titi, fika haraka kwa daktari mtaalamu na mzoefu wa kutambua saratani; fika kwake akufanyie uchunguzi mapema haraka iwezekanavyo. Unapoitambua kansa mapema, uwezekano wa kuitibu ni mkubwa sana. Na unapoichelewa uwezekano wa kukatwa titi na kifo ni mkubwa Sana.
Dalili zingine za saratani ya titi ni:
⚫ Kuvimba kwa titi lote au sehemu ya titi (hata kama hakuna kinundu kilichowazi/kinachoonekana)
⚫Muwasho wa ngozi .
⚫Maumivu ya titi (nipple pain),
⚫Kurudi ndani kwa chuchu (Nipple Retraction).
⚫Wekundu, kovu/baka (scaliness) au kujaa kwa titi au ngozi.
⚫Utokaji wa maziwa (tofauti na maziwa ya titi).
Wakati mwingine kansa ya titi inaweza kusambaa hadi kwenye mtoki (lymph nodes) kwapani (underarm) au hadi sehemu ya mfupa wa kola (collar bone) na kusababisha kinundu au kuvimba, hata kabla ya uvimbe wa awali kwenye titi haujahisiwa, lymph nodes lazima pia zipelekwe kwa daktari mtaalamu kwa ajili ya uchunguzi.
Kinga ni bora kuliko tiba. Na Kama tayari unayo saratani ya titi basi tuandikie email, bofya kiboksi cha bluu hapo juu kilichoandikwa "Send Email." Kisha tutumie maelezo yako tukupatie ushauri wa kitaalamu BURE!
kwa mawasiliano: +255768603979. “maamuzi yako ya sasa ni matokeo ya baadaye”
https://web.facebook.com/Yourhealthyourprioritylifestyles/…
https://paulbiswalo.blogspot.com/
https://www.pinterest.com/biswalopaul/
SHARE NA UNAOWAPENDA ILI WAFAIDI ELIMU HII YA BURE.
Ahsante na karibu sana.
No comments:
Post a Comment
warmly welcome
contact us via +255 768 603 979.