Health And Wellness Is Your Priority & Personal Development Mentorship Programs.

“Your health is your responsibility, love your health as you love your stuff”. -@Paul Biswalo.

We are looking forward to connect with you.

Our phone number is +255 768 603 979,for only calls/text &
+255 ,for WhatsApp only.
Email-address : biswalopaul@gmail.com.

It's me your lovely friend,
Yours in faithfulness,

-@Paul Biswalo, C.E.O & FOUNDER.
Mentor || Motivational Speaker || Trainer || Event Host || Entrepreneur || Healthy & Life coach || Presenter & Inspirational Public Speaker.
*let's meet all at the Top because is no longer crowded*

USHAURI JUU YA ULAJI WA MATUNDA.wasiliana nasi kupitia namba hii +255768603979. Maana ULAJI WA MATUNDA NI SULUHISHO KWA MAGONJWA SUGU KWENYE MIILI YETU.

======*******USHAURI JUU YA ULAJI WA MATUNDA*******======
**************************************************************************************

wasiliana nasi kupitia namba hii +255768603979. Maana ULAJI WA MATUNDA NI SULUHISHO KWA MAGONJWA SUGU KWENYE MIILI YETU.

Matunda yana faida nyingi mwilini na ni miongoni mwa vyakula vinavyopaswa kupewa kipaumbele katika milo yetu ya kila siku. Lakini kwa bahati mbaya, siyo watu wote wanaelewa umuhimu wa matunda na jinsi ya kula ili kupata faida zake.

 
 
Kutokana na kula matunda kinyume na utaratibu, watu wengi huyachukia matunda baada ya kujikuta wakiumwa tumbo au kujisikia kichefuchefu na kutapika mara baada ya kula. Wengine husikia tumbo kujaa gesi na kusikia kiungulia.

Halikadhalika, watu wengi wamefundishwa na kuzoeshwa kulishwa matunda baada ya mlo, mazoea ambayo ni kinyume kabisa na kanuni za ulaji sahihi wa matunda. Katika makala haya, utaelewa njia sahihi ya kula matunda ili kupata faida zake.

 

KULA MATUNDA TUMBO LIKIWA TUPU
===============================
-- Ili kunufaika na matunda, kula matunda wakati ukiwa na njaa na tumbo likiwa tupu. Unapokula matunda katika hali hii, matunda husagika haraka na virutubisho vyake husambaa mwilini kwa urahisi. Baada ya saa moja au zaidi, unaruhusiwa kula mlo wako mwingine kama kawaida.

USILE BAADA YA KULA
===================
-- Imezoeleka na watu wengi kula matunda baada ya mlo kamili. Hata kwenye hafla na tafrija kubwa mbalimbali, utaona matunda huliwa mwishoni baada ya chakula. HII SIYO SAHIHI na hayo ni makosa miongoni mwa makosa mengi yanayofanyika kwa sababu ya mazoea tu.

-- Inaelezwa kuwa ulaji wa matunda baada ya mlo siyo sahihi kwa sababu matunda huyeyuka haraka kuliko chakula cha kawaida. Tunda linapokuwa tayari kupita tumboni kuelekea kwenye utumbo mwembamba, huzuiwa na chakula. Baada ya muda tunda linachanganyika na chakula na kuoza na hatimaye kuzalisha asidi ambayo humfanya mtu kuumwa tumbo baada ya kula matunda. Lakini pia virutubisho vyake hupotea.



-- Ili kuepukana na hali hiyo ya msongamano kwenye tumbo, kula matunda saa moja kabla au kama utakula baada ya mlo, angalau kula baada ya masaa mawili. Ukila baada ya muda huo, utakuwa umetoa nafasi ya chakula kusagika na bila kuzuia uyayukaji wa matunda.

ZINGATIA KIWANGO CHA SUKARI KWENYE MATUNDA
===========================================
--> Baadhi ya matunda, kama vile papai, ndizi mbivu, yana kiwango kingi cha sukari, karibu matunda yote yana sukari, lakini mengine huwa na kiwango kingi zaidi. Hivyo inashauriwa kula matunda kwa kiwango cha wastani kila siku bila kuzidisha kiwango cha sukari cha gramu 25 kinachohitajika kwa siku.




--> Aidha, unapokula tunda, hakikisha unakula tunda kwa ukamilifu wake ili kupata virutubisho vyote. Kwa mfano unapokula chungwa, ni vizuri pia ukala pampoja na nyama zake ili kupata virutubisho vyote muhimu vilivyomo.

--> Jiwekee tabia ya kula matunda ya aina mbalimbali kwa nyakati tofauti ili kupata vitamini na madini tofauti tofauti kulingana na mahitaji ya mwili. Kwa kuwa matunda ndiyo yanayojenga na kuimarisha kinga ya mwili, ulaji wa matunda ya aina mbalimbali kutakuhakikishia mwili wako kinga imara dhidi ya maradhi na kamwe hutasumbuliwa na magonjwa mara kwa mara.

 
 
#FAIDA_ZA_LIMAO

Limao unaweza ukaliweka kwenye mboga au chakula kingine ili kuzipata faida zake .Pia unaweza kulipaka kwenye ngozi moja kwa moja.

Unaweza pia kupata virutubisho katika mfumo wa vidonge,vyenye mchanganyiko wa matunda mengi tofaut ikiwemo limao na machungwa vya kuongeza kinga ya mwili wako,kusaidia fizi zinazotoa damu, kuondoa harufu mbaya ya kinywa, kuzuia maumivu ya viungo,kuosha sumu ndani ya mwili na kusaidia uponaj wa vidonda ndani na nje ya mwili na kazi zingine nyingi.

Virutubisho hivi utatumia ndani ya mwezi mzima(vidonge 100,vitamu kama pipi) tunapatikana Tanzania nzima.







Tupate Elimu Juu PARACHICHI.

Parachichi ni tunda ambalo mti wake hujulikana kisayansi kama Persea amerikana. Tunda hili lina aminika kuwa na asili kutoka jimbo la Puebla, bara Amerika ya kusini kunako nchi ya Mexico. Ushahidi wa kale kabisa, takribani miaka 10000 BC umeonyesha parachichi lilitumika katika jimbo la Puebla nchini Mexico. Lakini kutokana na faida nyingi kiafya zipatikanazo kwa ulaji wa tunda hili, tunda hili sasa hupatikana na kutumika kwa lishe sehemu nyingi duniani hususani barani Afrika.
Parachichi ni tunda la pekee ukilinganisha na matunda mengine, kimsingi matunda mengine huwa yana wanga(carbohydrate) kwa wingi, wakati parachichi lina aina ya mafuta ambayo yana faida kwa afya.




Parachichi katika tafiti nyingi limeonekana kuwa na faida katika afya ya moyo. Wagonjwa wa moyo wamekuwa katika makatazo ya kutumia aina ya mafuta ambayo yamekuwa yakichangia kuongezeka kwa lehemu katika damu(mafuta hayo kitaalam kama polysaturated fat), na kuongeza matumizi ya mafuta yasiyoongeza lehemu katika damu (monosaturated fat). Parachichi ni chanzo kizuri cha mafuta yasiyoongeza lehemu katika damu. Utafiti unaonyesha kuwa matumizi ya mafuta haya katika parachi hupunguza lehemu iliyo hatari ( kitaalam kama, Low density lipoprotein), na huchangia katika ongezeko la lehemu isiyo hatari( High density lipoprotein).




































Madini ya Potasiamu ni aina ambayo huwa watu hawapati ya kutosha kutoka katika vyakula. Parachichi lina kiwango kikubwa cha madini ya potassium kuliko ndizi. Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa matumizi ya madini haya huambatana na kupungua kwa shinikizo la damu, shinikizo la juu la damu laweza kupelekea mtu kupata kiharusi, shambulizi la moyo hata figo kushindwa kufanya kazi.


Parachichi lina kiwango kikubwa cha fiba. Fiba ni kirutubisho kutoka katika vyakula vya jamii ya mimea, fiba huwa hazimeng’enywi tumboni lakini huwa zina umuhimu mkubwa sana, kama kusaidia kupunguza uzito wa mwili, kusaidia urekebishaji wa kiwango cha sukari mwilini na kupunguza hatari ya kupata magonjwa mengi mwilini. Kuna aina fulani ya fiba ambazo huwa ni virutubisho kwa ajili ya bakteria wenye faida tumboni, hii huimarisha kinga ya mwili na kusaidia mwili kufanya kazi katika kiwango kinachotakiwa. Kwa kuwa parachichi lina kiwango kikubwa cha fiba, husaidia kuboresha mmeng’enyo na kupata choo katika hali ya kawaida.


Aina ya mafuta na virutubisho tulivyoviona awali katika parachichi vinasaidia afya ya ngozi yako. Husaidia ngozi yako kutokuwa kavu na kuwa na unyevu unaotakiwa na kuifanya ngozi kuwa laini na yenye afya. Vitamini C husaidia katika kusaidia uponaji haraka wa ngozi na kujijenga upya kwa seli za ngozi zilizoharibika,husaidia kujenga elastini na collageni ambazo ni muhimu katika ngozi. Uwepo wa virutubisho viondoavyo sumu(antioxidants) katika parachichi kama carotenoidi na vitamini E, hutusaidia kutukinga na mionzi mikali ya jua, kwa hiyo huzuia makunyanzi katika ngozi na kuifanya ngozi yako kuwa na mwonekano mzuri wakati wote.


Tunda hili ni lishe bora kwa wale wenye kisukari. Parachichi lina kiwango kidogo cha sukari ukilinganisha na matunda mengine. Pia uwepo wa mafuta aina ya ‘monosaturated’ husaidia kuboresha ufanyaji kazi wa homoni ya insulini, katika urekebishaji wa kiwango cha sukari mwilini. Faida nyingine ni kuwa Vitamini C katika parachichi husaidia kuimarisha mishipa ya damu na kuboresha kinga ya mwili ambayo ni faida kubwa kwa wagonjwa wenye kisukari.


Faida katika afya ya uzazi ni dhahiri. Parachichi lina Vitamini E ambayo ni “antioxidant” Potasiamu, Vitamini B6,Vitamini C ambazo hutusaidia kutukinga na magonjwa ya moyo hata yale ya kisukari. Chochote kile kinachosaidia afya ya moyo pia husaidia afya ya uzazi. Wanaume wenye magonjwa ya moyo na kisukari huwa tatizo kubwa la upungufu wa nguvu za kiume.
 
Parachichi pia limeonekana kuwa na faida nyingi katika kuboresha afya ya macho, viungo vya mwili na nyinginezo nyingi. Katika utafiti mmoja uko Marekani, ulionyesha kuwa watu walao parachichi walionekana kuwa na afya bora ukilinganisha na wale wasiokula parachichi. Waliokula parachichi hawakupatwa na matatizo ya mmeng’enyo ukilinganisha na wale wasiokula. Matatizo ya mmeng’enyo huchangia watu kupatwa na magonjwa ya moyo na kisukari.


Hapo ni kwa mafupi tu, Ila kwa ushauri Tuwe tunapendelea kutumia matunda mara kwa mara ili kuweza kupata faida za kiafya na kuboresha miili yetu dhidi ya matatizo madogo madogo ambayo yakikua yanakua ni makubwa na yasiyokua rahisi kuyakabili.
Ukienda sokoni usisahau parachichi a.k.a Avocado.

 
 
#BAADA_YA_CHANGAMOTO_KUIKUMBA_JAMII_JOPO LA WATAALAMU/MADAKTARI_WALIOBOBEA_KATIKA AFYA_YA_MWANADAMU_WALIFANYA_TAFITI_YA_NAMNA_
YA_KUONDOA_CHANGAMOTO_HIZO_BILA_KUTUMIA_DAWA_AU_
VIAMBATA_VYENYE_SUMU_BALI_KUTUMIA_VIRUTUBISHO.

Virutubisho hivyo vimekuwa vikitumiwa na watu wengi kwa zaidi ya mataifa 170 duniani na tunashuhuda nyingi za watu waliopata kuboreshwa kwa afya zao baada ya kutumia virutubisho hivyo.

Kwa Ushauri au Kupata Huduma zetu Kama Uko Dar Es Salaam,Dodoma,Arusha,Mwanza Na Mbeya,Rukwa,Katavi,Singina,Ruvuma,Njombe,Simiyu,Mara...na Popote Ulipo(Tanzania Na Zaidi Ya Nchi 160 Duniani).

Kwa maelezo zaidi jinsi unavyoweza kupata bidhaa zinazo ondoa tatizo hilo wasiliana nasi kupitia namba hii +255768603979.

Free delivery ndani ya Dar, kama upo mkoani utatumiwa pia ndani ya tanzania.
Ni virutubisho asili ambavyo vimeshawasaidia watu wengi saana hapa nchini na Duniani kwa Ujumla. Karibu Upate huduma zetu kwa ushauri pia wasiliana nasi PIGA /TUMA NENO :"Health and wellness is Your Priority".kisha #ULAJI WA MATUNDA NI SULUHISHO KWA MAGONJWA SUGU KWENYE MIILI YETU.

kwa mawasiliano: +255768603979“ maamuzi yako ya sasa ni matokeo ya baadaye”.
https://web.facebook.com/Yourhealthyourprioritylifestyles/
https://paulbiswalo.blogspot.com/
https://web.facebook.com/MaishaNiAfyaLindaAfyaYako/
https://www.pinterest.com/biswalopaul/

SHARE NA UNAOWAPENDA ILI WAFAIDI ELIMU HII YA BURE.
KWA KUENDELEA KUPATA UP-DATE JUU YA AFYA LIKE PAGE HII NA KUSHARE ELIMU HII YA BURE KWA WENGINE.  


 
Share:

No comments:

Post a Comment

warmly welcome

contact us via +255 768 603 979.

Popular Posts

Blog Archive

for any assistance.

“Your health is your responsibility, love your health as you love your stuff”. -@Paul Biswalo.

We are looking forward to connect with you.

Our phone number is +255 768 603 979,for only calls/text &
+255 ,for WhatsApp only.
Email-address : biswalopaul@gmail.com.

It's me your lovely friend,
Yours in faithfulness,

-@Paul Biswalo, C.E.O & FOUNDER.
Mentor || Motivational Speaker || Trainer || Event Host || Entrepreneur || Healthy & Life coach || Presenter & Inspirational Public Speaker.
*let's meet all at the Top because is no longer crowded*

Featured post

UNAFAHAMU UMUHIMU NA FAIDA YA KUBORESHA KINGA YA MWILI??????

AFYA YAKO NI JUKUMU LAKO. UNAFAHAMU UMUHIMU NA FAIDA YA KUBORESHA KINGA YA MWILI?????? jiulize swali hili na utafakali vizuri ilik...

Followers

Contact Form

Name

Email *

Message *

Labels

Total Pageviews

Theme Support